THOMAS MULLER
Watu hawaangalii umeishi miaka mingapi ila umeleta mabadiliko gani kwenye jamii na ulimwengu mzima.
Miaka
ni namba tu ni kama vile ndani una ndoo kubwa lakini haina maji ila
mwenzako mwenye kikombe tu lakini kimejaa maji hivyo mwenye maji ana
thamani kubwa sana kuliko asiye na maji, msemo huu utauelewa siku ukiwa
na kiu.
Muller
mzaliwa wa 89 mwenye miaka 24 tu lakini ashafanya mambo makubwa kimpira
kuliko watu wengi waliostaafu mpira wakiwa na miaka zaidi ya 36.
Dunia
nzima macho yetu yapo Brazil licha ya utofauti wa rangi, dini, kabila
na itikadi lakini linapokuja suala la kombe la dunia watu wote hujumuika
pamoja na ndiyo maana unaambiwa mpira si vita bali burudani.
Si
kila timu ishacheza lakini ukianza ushaweka historia, alianza Marcelo
kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli katika mashindano
haya ya mwaka 2014 na mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kufunga
goli la kwanza la kujifunga ingawa ni kwa mabaya lakini mtu ashaandika
historia yake na itabaki hivyo vizazi na vizazi.
Robin
Van Persie hadi sasa ndiyo kafunga goli bora ambalo hata uwe unamchukia
lazima utamani kuwa na mshambuliaji wa aina yake maana kwa lugha ya
kigeni wanasema "World Class Player" yaani mchezaji mwenye uwezo wa dunia na mwenye sifa zinazohitajika.
Wapo wengi waliokwisha kuweka rekodi zao ila kwa jana usiku ni THOMAS MULLER ndiye aliyeweka rekodi.
Thomas Mulller - Mshambuliaji wa Ujerumani
Muller
ndiye mchezaji wa kwanza kufunga hat trick yaani goli tatu katika mechi
moja katika kombe la dunia la mwaka huu kule Brazil hivyo na kumfanya
mpaka sasa kuongoza katika orodha ya wafungaji katika mashindano hayo
kwa kuwaacha kwa goli moja wanaomfuatia kama vile Robin Van Persie,
Neymar pamoja na Karim Benzema.
Katika
fainali za mwaka 2010 kule Afrika ya Kusini, ,uller ndiye alikuwa
mfungaji bora wa mashindano yale na kwa jinsi alivyo na uchu wa mabao
anaweza kutetea kiatu chake kutokana na kuzungukwa na watu wenye vipaji
na viungo bora kabisa ulimwenguni.
Pia
Muller bado mabao mawili tu ili awe mfungaji bora wa Ujerumani wa muda
wote kitu ambacho ni rahisi sana kwake kukifikisha na sitoshangaa kama
atazidi magoli sita zaidi.
Huyu
ndiye Thomas Muller Mjerumani mwenye roho ya paka aiyekubali kushindwa
ndiyo maana hata klabu yake ya Bayern Munich waligoma kumuuza na
kuonmgezea mkataba kutokana na kipaji na umuhimu wake katika klabu.