Jumla ya Mara Iliyotazamwa

6 Okt 2014

KINANA ATINGA IRINGA, ASEMA UCHAGUZI UJAO WAPINZANI WATAPUKUTIKA


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa skafu, baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Vijijini, leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga na Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Isimani William Lukuvi wakati wa mapokezi hayo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mbunge wa Kilolo Profesa Peter Msola wakati wa mapokezi hayo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa, Asas





DIAMOND AFANYA MAKAMUZI YA NGUVU BIG BROTHER HOTSHOTS


Diamond Platnumz akifanya makamuzi ndani ya Big Brother Hotshots. 

STAA wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku huu amefanya makamuzi ya nguvu katika uzinduzi wa shindano la Big Brother Hotshots unaofanyika jijini Johanessburg nchini Afrika Kusini. 

Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na watu wawili mrembo Irene 'La Veda' na Idriss. Jumla ya washiriki 26 kutoka mataifa 12 ya Afrika watachuana kwa siku 63 kutafuta mshindi atakayejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 300,000.

UNDANI WA KIFO CHA MKE WA ALICHOKI HUU HAPA ,CHEKI PICHA


Stori: Gladness Mallya
Majonzi! Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki, marehemu Shuea Hamis ‘Mama Shuu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, Choki alisema kwamba mke wake ameugua kwa muda wa miezi tisa akisumbuliwa na tatizo la mguu.
Alisema kwamba katika jitihada za matibabu, mkewe huyo alitibiwa nchini India ikashindikana, akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Ukweli nimeumia kwani alikuwa ni mshauri wangu mkuu na ndiye alikuwa kila kitu kwangu.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
Ali Choki akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe enzi za uhai wake.
Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwake tangoma, kigamboni jijini dar na mazishi ya mkewe yalitarajiwa kufanyika jana juma pili sa 10:00 jioni katika Makaburi ya Maduka Mawili, Changombe Dar.