Stori: Gladness Mallya
Majonzi! Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Majonzi! Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki, marehemu Shuea Hamis ‘Mama Shuu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, Choki alisema kwamba mke
wake ameugua kwa muda wa miezi tisa akisumbuliwa na tatizo la mguu.
Alisema kwamba katika jitihada za matibabu, mkewe huyo alitibiwa nchini
India ikashindikana, akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku
wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Ukweli nimeumia kwani alikuwa ni mshauri wangu mkuu na ndiye alikuwa kila kitu kwangu.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwake
tangoma, kigamboni jijini dar na mazishi ya mkewe yalitarajiwa kufanyika jana juma pili sa 10:00 jioni katika Makaburi ya Maduka Mawili, Changombe Dar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni