Jumla ya Mara Iliyotazamwa

21 Ago 2014

UVCCM MKOA WA IRINGA KUMSIMIKA KAMANDA WAKE MH. SALIM ASAS 23/08/2014

Maandalizi ya shuhuli ya kumuapisha KAMANDA wa UVCCM MKOA WA IRINGA MH SALIM F. ABRI (ASAS) yamekamilika na wageni nyote mnatakiwa kufika IRINGA siku ya kesho ijumaa 22/08/2014. Ulizi WA uhakika na Amani ya kutosha ipo.

Maandalizi yote hayo ni chini ya KAMANDA bora SALIM F. ABRI (ASAS)

Tunawatakia safari njema ya ujio wa IRINGA karibuni sana.

UNYAMA WA KUTISHA IRINGA MWANAFUNZI AUA MTOTO WAKE WA SIKU MOJA AMHIFADHI KATIKA MFUKO WA RAMBO













Na Mathias Canal-Iringa

Mwanafunzi Vema  Mtati wa chuo cha unesi Chimala wilayani Mbarali mkoani Mbeya akamatwa na polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za mauwaji ya mtoto wa siku moja aliyejifungua salama.
Tukio hilo la kinyama limetokea leo saa 12 jioni  katika  eneo la Kijiweni kata ya Mvinjeni Manispaa ya Iringa kutokana na baadhi ya majirani kufichua siri hiyo nzito ya kuwepo kwa jaribio za binti huyo kufanya mauwaji hayo. 

Mmoja kati ya majirani aliueleza kuwa binti huyo mwanafunzi akiwa na mimba ya miezi tisa alifika katika nyumba hiyo kwa rafiki yake ambae ni mfanyakazi wa bar mmoja eneo la vibanda vya CCM mjini Iringa aliyefahamika kwa  jina la Joys siku kama tano kabla ya usiku wa jana kujifungua salama katika chumba hicho.

Shuhuda  huyo  alidai kuwa mapema  asubuhi ya  leo  walisikia  sauti ya  mtoto  mchanga akilia   huku sauti ya radio  ikipandishwa  kupoteza  sauti ya  mtoto  huyo  ili  wapangaji  wengine  wasijue suala  hilo.
Hivyo  kutokana na hali  hiyo ndipo waliamua  kufika  ofisi za mtandao huu kufichua siri hiyo kwa maombi ya kutotajwa popote  jina la  shuhuda  huyo.

" Mimi ni  raia mwema na mwanamke  mwenye  uchungu  nimekuja kwako huku  nikijua hutatoa siri  hii ...katika  nyumba ambao naishi  kuna  mwanafunzi amejifungua mtoto jana usiku na kwa  sasa amejifungia ndani na  mwenye chumba anaitwa Joys anafanya kazi  vibanda  vya CCM sasa  lengo  la kujificha nafikiri ni kutaka  kufanya jaribio la kuua mtoto  huyo  sasa naomba usaidie  kuokoa maisha ya mtoto  huyo unatusaidiaje na sisi kwenda  polisi tunaogopa ushahidi"

Kutokana na maelezo hayo  yasio na chembe  ya uongo mtandao  huu ulipiga  simu kwa OCD Iringa Bw Pyuza na  bila  kuchelewa kikosi kazi  akiwemo askari wa dawati la jinsia  kilifika  katika ofisi  za mtandao  huu wa matukiodaima na safari ya  kufuatilia  suala  hilo  ilipoanza kwa kumkamata mwenyeji wa mwanafunzi huyo ambae ni mmiliki wa  chumba kisha  kupokonywa  simu yake ili asifanye  mawasiliano nyumbani na baada ya hapo kwenda katika nyumba  husika .
Hata  hivyo ukweli wa jambo ulianza kujionyesha baada ya kufika katika  chumba  hicho na  kukuta mlango  umefungwa kwa ndani na baada ya  mwenye chumba kugonga ndani mwanafunzi huyo aliigiza kuwa alikuwa akifanya usafi  ila baada ya  kuhojiwa na polisi alidai kuwa kwa sasa ana mtoto mmoja ambae  yupo  kijijini Magulilwa  wilaya ya Iringa .

Uchunguzi wa  kipolisi ulianza na kikosi  hicho kwa maswali ya kiuchunguzi na ndipo alipokiri kuwa anamtoto mwingine ambae amejifungua usiku wa  leo na amemhifadhi  katika mfuko wa rambo ndani chini ya kitanda .

Alipotakiwa  kumtoa  alifanya  hivyo na polisi  na mmiliki wa mtandao  huu kushindwa  kujizuia kuangua  kilio kutokana na kile  walichokiona  kutoamini .

Mtoto  huyo alikutwa amekufa huku akiwa amefungwa na  nguo nyingi  pamoja na kumwagiwa vumbi ya mkaa na chumvi  ili asitoe harufu na kufungwa  vizuri katika mfuko wa rambo mweusi  kisha kuwekwa katika mfuko mkubwa wa  salfeti tayari kwa  kuvuta  subiri ya kwenda kumtupa mtoto  huyo porini .

KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM MKOA WA ARUSHA CHAKUTANA KUMJADILI NAIBU KATIBU UVCCM MKOA

???????????????????????????????
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Arusha Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano huo ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha waliaofikiana kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi mabaya ya fedha za umoja huo.
???????????????????????????????
Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu Ally Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga marufuku Kaimu Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe na kazi za UVCCM mkoa wa Arusha.
CCM 1
Mwenyekiti wa UCVVM Mkoa wa Arusha Robnson Meitinyiku  na baadhi ya wajumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakisikiliza maazimio yaliyopitishwa na wajumbe wakati yalipokuwa yakisomwa mbele ya waandishi wa habari mjini hapa
CCM 2
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi katikatika pamoja na wajumbe wenzake wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande wake alitoa ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua watendaji lie linaangalia watendaji wenye sifa.
CCM 3
Sehemu ya mkutano wa waandishi wa habari na wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kikiendelea leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose
???????????????????????????????
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatulia maazimio yaliyofikiwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha kilichofanyika leo jioni.Ambapo Baraza hilo liliazimia kuanza kufanyiak kwa ukaguzi wa mara kwa mara katika ofisi za UVCCM mkoa kwa kila mwezi kwa ajili ya kdhibiti ubadhilifu.
???????????????????????????????
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini ajenda za kikao hicho, ambapo Baraza hilo lililaani kitendo cha Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa cha kufunga ofisi ili Kamati ya Utekelezaji isifanye kikao ambacho walikubaliana pia kitendo cha kukwepa kuitisha vikao licha ya kukubaliana  na Mwenyekiti kama kanuni inavyotaka na kuuotosha umma kwamba Kamati ya Utekelezaji ndio iliyofunga ofisi.
???????????????????????????????
???????????????????????????????
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Robson Meitinyiku akifuatilia kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha kilichofanyika leo jijini hapa na kupitia maazimio ya kumtaka Katibu wa CCMM Mkao Mary Chatanda asiingilie Jumuiya hiyo bali awe mshauri kupitia bvikao vya jumuiya ambapo yeye ni Mjumbe katika vikao vya Utekelezaji na vya Baraza.
???????????????????????????????
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia maazimio yaliyokuwa yakisomwa mbele ya wanahabari leo mjini hapa ambapo Baraza hili liliazimia kwamba endao Katibu wa Mkoa Mary Chatanda atabainika kuwa na ubadhilifu basi asihamishwe mkoa mwingine na apelekwe mahakamani ili iwe fundisho.

KAMATI KUU YA CCM YASISITIZA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UENDELEE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi alisema,
Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, ilipokea taarifa na kufanya tathimini juu ya maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini, ndani na nje ya Bunge.
Kamati Kuu vilele imepokea na kujadili taarifa kuhusu mazungumzo na mashauriano kati ya vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR-MAGEUZI  na CCM. Mazungumzo ambayo yalisimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini.
Aidha Kamati Kuu ilipokea pia taarifa ya kikao cha Baraza la Vyama vya siasa na pia taarifa ya kikao cha Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD). Vikao hivyo vyote vilihusu maendeleo ya mchakato wa Katiba nchini.
Kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba, Kamati Kuu imearifiwa maendeleo ya majadiliano na upigaji kura katika kamati za Bunge hilo. Kwa ujumla Kamati Kuu imeridhishwa na namna wajumbe wa Bunge Maalum wanavyoshiriki katika kujadili na kujenga hoja na wanavyoshughulikia tofauti za kimtazamo na kimawazi katika vikao vyao na hatimaye uhutimishaji wa majadiliano kwa kura.
Kamati Kuu inawahimiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kuhudhuria vikao vya kamati na vile vya Bunge na kushiriki katika mijadala kwa kutanguliza masilahi mapana ya taifa na hatimae kuipatia nchi katiba inayotarajiwa na watanzania wote. Chama Cha Mapinduzi kinautakia kila lakheri mchakato huu.
Aidha Kamati Kuu imeridhishwa na juhudi za vyama na wadau mbalimbali katika kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano kwa lengo la kupata muafaka. Hata hivyo Kamati Kuu imesikitishwa na kuvunjika kwa mazungumzo kati ya CCM, CUF,CHADEMA na NCCR-MAGEUZI yaliyokuwa yanasimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kengo la kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano ili kupata muafaka.
Kamati Kuu imepokea na kuridhishwa na taarifa kuhusu juhudi zinazofanywa na Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD) pamoja na vyama vinavyounda TCD katika kutafuta muafaka wa kisiasa kwa lengo la kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na kuaminiana kati ya wadau mbalimbali na hasa kati ya vyama vya siasa.
Kamati Kuu inaunga mkono juhudi za TCD za kuendeleza mashauriano kati ya vyama na ndani ya vyama kwa lengo la kupunguza mivutano, kujenga uaminifu na ustahimilivu na umoja kati yao.
Hivyo Kamati Kuu imempongeza Katibu Mkuu wa CCM kwa namna alivyoshiriki na kukiwakilisha Chama kwenye vikao hivyo.
Kamati Kuu imemuagiza Katibu Mkuu aendelee kukutana na vyama na wadau wengine katika kufanikisha lengo la maridhiano hayo.
Mwisho Kamati Kuu inaendelea kuwasihi Watanzania wote kuendelea kushikamana na kuvumiliana pale wanapopishana kimtazamo juu ya hoja mbalimbali za katiba kwani Amani,  Utulivu na Utanzania wetu ni muhimu kuliko tofauti zetu za kimitazamo. Mchakato wa Katiba nchini uendelee kuwa fursa ya kuijenga nchi yetu badala ya kutumika kutugawa na kututenganisha.

HIZI NDIZO PICHA ZA ANTI EZEKIEL GUMZO MITANDAONI KWA JIONI HII





VANESSA MDEE VS JOKATE MWEGELO NANI KIMODO WA MAANA??

They are both smart, classic, intelligent, talented, educated and they both have natural beauty.



Frankly speaking those chicks are cute but there is something ambacho mmoja kamzidi mwenzie je wewe unadhani ni kipi?

HABARI PICHA: MFAHAMU BABY MAMA WA PROFESA JAY, "MAMA LISSA"


Profesa Jay amemuonesha mwanamke ambaye anaweza kuwa Mrs. Joseph Haule ambaye amemtaja kama mama mtoto wake.
Kupitia Instagram, Profesa amepost picha akiwa na mwanamke huyo na kuandika, “OF COURSE ni Baba LISA na Mama LISA. .... What more can I SAY?? #MWANALIZOMBE.”

UNAAMBIWA DEVOTA YU MBIONI KURITHI MIKOBA YA MTITU.






BAADA ya hivi karibuni Katibu wa Bongo Movie Unity, William Mtitu kutangaza kujiuzulu na kuiacha nafasi hiyo wazi, Katibu Msaidizi, Devota Mbaga amefunguka kuwa anajiandaa kushika nafasi na kwamba kujiuzulu kwake hakusaidii chochote kwani wanachama wanahitaji fedha.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Devota Mbaga.

Akistorisha na paparazi wetu Devota alisema hatua ya Mtitu kujiuzulu haisaidii kitu, wanachama wanahitaji fedha ambazo wamekula kwani alitangaza kujiuzulu baada ya kuambiwa aweke mezani fedha walizokula.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William J. Mtitu akitabasamu ndani ya studio za Global TV Online.
“Najiandaa kushika wadhifa huo kufuatia Mtitu kuachia nafasi baada ya kuambiwa aweke mezani fedha walizokula, amefanya hivyo, ili aonekane msafi arudishe fedha au aje awaombe msamaha wanachama,” alisema Devota.

PICHA: UNAAMBIWA HUU NDIO MKOKO ANAOMILIKI MTOTO WA KAJALA, TAZAMA HAPA NI SHIDAAAH!!!



Unaambiwa dogo hivi sasa anamiliki bonge la ndinga kama inavyoonekana kwenye picha, kweli noma sana

JE, WAJUA?! JAQUELINE WOLPER ANAONGOZA KWA KUBADILI NAMBA ZA SIMU!KISA?! KUNA NINI NA KWANINI?! SOMA ZAIDI HAPA!

KUNA nini kwani? Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper anatajwa kuongoza wasanii wenzake kwa kubadili namba za simu za mkononi huku baadhi ya mashoga zake wakijiuliza kulikoni?
Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper.
Kwa mujibu wa rafiki mmoja wa karibu na Wolper (jina lipo), anamshangaa sana shoga yake huyo kwani amekuwa akibadili namba za simu kwa mwaka mmoja hata mara saba.
“Unajua kwa maisha ya sasa, simu ikipotea mtu unairinyuu laini yako ileile, maana ndiyo inayojulikana na wadau. Lakini yule mwenzetu siyo. Nimeshamsevu kwenye simu yangu kwa majina ya Wolper, Wolper Tena, Wolper Nyingine, Wolper Nyingine Kabisa na Wolper Hakuna Tena, lakini zote kwa sasa hazipo hewani,”
alisema shoga yake huyo huku akicheka
Wolper alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi iliyozoeleka, hakupatikana. Jitihadi zilifanyika akaja kupatikana kwenye namba mpya ambapo alisema:
“Mimi nikishapoteza laini naona uvivu kwenda kuirinyuu, ndiyo maana nanunua nyingine.”

KUMBE PAMOJA NA MBWEMBWE ZOTE ZILE KUMBE MASOGANGE ANAUZA BAR SOUTH AFRICA, HUU HAPA USHAIDI WOTE

Noma sana uaambia kumbe masogange anauza bar mwenzie hamisa mobeto amempiga vijembe kwa kuweka video ikimuonyesha akiwa kazini itazamae hapa.




Mfahamu mwanamke mfupi zaidi duniani 'Sentimita 60' anaepata deals kubwa Marekani


Unaweza kuwa mfupi kiasi cha kukufanya utamani kuongezeka, lakini ukiwaona wenzako wanavyopeta nalo basi utagundua unapaswa kumshukuru Mungu kwa umbo lolote ulilopewa.
Jyoti Amge, mwenye umri wa miaka 21, ndiye mwanamke mwenye kimo kifupi zaidi duniani akiwa na urefu wa inches 24 (sawa na urefu wa rula mbili za sentimita 32).
Jyoti ambaye ni mkazi wa Napur, India, aliingia rasmi katika kitabu cha Guinness mwaka 2011 kama mwanamke mfupi zaidi duniani aliye hai na tayari ameshapata deals kubwa kwa kimo chake.
Amewahi kushiriki katika makala maalum ya Body Shock: Two Foot High Teen na August 13, na mwaka huu alipata deal ya kuigiza katika ‘American Horror Story: Freak Show’.

Mwanamke huyo ambaye kimo chake kinatajwa kuwa kimetokana na tatizo la kutokua kawaida ‘achondroplasia’ anaendelea kupiga deals kubwa na amegeuka kuwa lulu kwa muonekano huo wa kipekee.

Jyoti akiwa amebebwa

20 Ago 2014

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA FAMILIA YA JAJI MAKAME

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Agosti, 2014.
 Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Agosti, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Agosti, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto wa marehemu pamoja na Jaji Mstaafu Mark Bomani alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Agosti, 2014.

PICHA NA IKULU

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye ukumbi wa NEC Dodoma ,akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na mjumbe mwenzake Samia Suluhu Hassan muda mfupi kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hakijaanza kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Oganizesheni Dk.Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM DK. Salim Ahmed Salim ndani ya ukumbi wa mkutano wa White House kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Profesa Anna Tibaijuka, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Dodoma.(Picha na Adam Mzee)