Jumla ya Mara Iliyotazamwa

18 Ago 2014

JAJI LEWIS MAKAME AFARIKI DUNIA


Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame, amefariki dunia.

Habari zilizotupikia zinaeleza kwamba, Jaji Makame amefariki katika hospitali ya AMI Trauma Centre iliyoko Masaki jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa tangu Julai mwaka huu.


Hii ilikuwa Julai 28, 2014 wakati Rais Jakaya Kikwete alipokwenda kumjulia hali Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Lewis Makame aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya AMI iliyoko Masaki jijini Dar es Salaam l (Picha na Freddy Maro - Julai 28, 2014)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni