Miongoni
wa makundi ya vijana hasa wenye umri wa kati miaka 15-23 wengi wao
huota wakifanya mapenzi ndotoni, lakini mbali na hao kuna watu wazima
pia ambao hukumbwa na tukio hili. Uotaji wa ndoto hii umekuwa
ukitafsiriwa na wengi kwa maana tofauti tofauti, huku wengine
wakiuhusisha na ufanyaji mapenzi na Majini.Uchunguzi unaonyesha kuwa
uotaji ndoto za kimapenzi huwatokea hata watu ambao hawajawahi kufanya
kitendo hicho kabisa, huku watu wanaofanya nao wakiwa ni wale
wanaowafahamu kwa sura au wasiowafahamu. Wengi wamekuwa wakijiuliza
maswali mengi juu ya nini kinachangia uotaji huu wa ndoto za
kimapenzi?
Kitaalamu ndoto hizi hutokana na mawazo ya mtu husika ambayo
yanaweza kugawanywa katika sehemu mbili ambazo ni MAWAZO YALIYO WAZI au
YALIYOJIFICHA. Mtaalamu wa masuala ya ndoto Daktari Gillian Holloway
anaeleza kuwa ndto hizi hufumbua maamuzi na hisiazilizojificha nyumba ya
ubongo.Pamoja na tendo hili kuwa baya katika mitazamo ya wengi hasa
kiimani, lakini bado si kitaalamu halina ubaya kwa kiwango hichokwani
mara nyingine husaidia kutafsiri yale ambayo wahusiakahawakupata
kuyafahamu kabla. Kwa mfano vijana ambao hawajafanya mapenzi hupata
kutambua raha itokanayo na kitendo hicho na hivyo kuwaamshia hisia za
kimapenzi ambazo pengine hawakuwa nazo hapo
awali.Wachunguzi wa masuala
ya ndoto wanasema ndoto hizi zikitumika vizuri zinaweza kusaidia kumpata
mchumba anayegusa hisia za moyo, aina ya mapenzi yanayokufurahisha,
haiba ya mpenzi umpendaye na wakati mwingine huchangia kuongeza
uzalishaji wa homoni na kupunguza msongo wa mawazo sawa na mtu
aliyefanyamapenzi kihalisia.Hata hivyo watu wanaotajwa kutokewa na
kitendo hicho marakwa mara ni wenye tabia ya kuogopa wanaume/wanawake na
hivyo kuzikandamiza hisia zao, wanaochochea hamasa za kingono
kutokuzikata, (mfanokufanya romance na kuachana bila kuingiliana),
wanaotazama picha za ngono, wanaozungumzia sana mambo ya kimapenzi na
wale wanaowaza sana wapenzi wao walio mbali.Kwa maana hiyo ili mtu
asiweze kutokewa na ndoto hizo hana budi kujizuia na mambo hayo
yanayotokana na uamshaji na ukandamizaji wa hisia za kingono. Hii ina
maana ya utashiwa mtu wa kutopenda kuota, lakini sia
kwamantiki kuwa
uotajihuu unauhusiano na mambo ya kishirikina au kichawi kama ambavyo
watu wengine wanavyoaminishwa.Mwisho kama kuna wanaodhani kuwa ndoto
hizi zimewadhuru kwa namna moja au nyingine, wafahamu kuwa
kilichowadhuru si kuota ndoto hizo bali ni wasiwasi wao unaotokana na
kusikia na wala si madhara kwa maana ya kuota kwenyewe, kwani ikiwa ni
ndoto hata wanyama kama Mbwa, Paka na Sungura nao huota wakifanya
mapenzi, ushahidi ambao unatosha kutupilia mbali hoja yandoto kutokana
na majini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni