Jumla ya Mara Iliyotazamwa

20 Ago 2014

TAARIFA KUTOKA BODI YA MIKOPO KWENDA KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU!


Bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania imeanzisha mpango mpya kwa ajili ya kupambana na uhaba wa Walimu wa masomo ya Sayansi na hesabu wa shule za msingi kwa kutoa mikopo kwa Wanafunzi wa ngazi ya stashahada (Diploma) watakaochaguliwa.
Ni mpango maalum unaoanza mwaka huu wa masomo 2014/2015 ambapo Mkurugenzi msaidizi wa habari, elimu na mawasiliano Cosmas Mwaisobwa amesema huu mpango utasaidia Wanafunzi zaidi ya elfu tano. 
Maneno yake mengine ni haya:  ‘ Serikali inafanya jitihada za kuziba pengo la uhaba wa Walimu wa hayo masomo kwenye shule za msingi na sasa hii imekua programu maalum itakayoendeshwa na chuo kikuu cha Dodoma mwaka huu‘

Pamoja na hayo bodi imekiri kuchelewesha kuwalipa fedha za vitendo wanafunzi wa vyuo vitano mwezi July 2014 kutokana na changamoto ya uhaba wa fedha lakini ahadi ni kuwa malipo hayo yatafanywa hivi karibuni.


Wanachuo hao ni kutoka Tumaini Makumira wanafunzi 1715, Stephano Moshi 1191, IFM 2578, Mt. Agustino 2639, Teophilo Kisanji Mbeya ni Wanachuo 1823 ambapo jumla ya Wanachuo hao inafikia 9946.

Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Wanafunzi ambao wamecheleweshwa kulipwa hela za mafunzo kwa vitendo, mpaka wiki ijayo malipo yao yatakua tayari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni