Jiwe
hili lipo katika kata ya ilima, nje kidogo ya mji wa Tukuyu Mbeya
katika barabara ielekeayo Kyela, ni jiwe ambalo juu yake kuna chuma
ambacho hakijafungwa kwa nati wala kitu chochote lakini hakitikisiki
wala hakitoki.
Inasemekana jiwe hili liliwekwa enzi za ukoloni na koloni la mwingereza.
Miaka
kadhaa iliyopita wananchi wa eneo hili walitaka kujua chini ya jiwe
kuna nini? ndipo walipoamua kuchimba ili kujua kuna nini lakini
hawakukuta kitu chochote.
Baada
ya kukuta hakuna kitu chochote ndipo walipotaka kuliangusha ili
lisiwepo kabisa walijaribu kutaka kuliangusha pasipo mafanikio kwa
sababu halikuonesha mwisho wake ni wapi kwa kwenda chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni