Jumla ya Mara Iliyotazamwa

18 Ago 2014

Picha: Utengenezaji wa video ya Profesa Jay 'Tatu Chafu', asema madirector wetu wakiwezeshwa wanaweza


Profesa Jay ameanza kushuti video ya wimbo wake ‘Tatu Chafu’ alioutoa wiki chache zilizopita ukiwa umetayarishwa ndani ya studio za Mwanalizombe.
Katika video hiyo, tarajia kumuona profesa akiwa na katika maisha ya hali ya juu, gari la kifahari 'Hammer', Cigar mtoko wa ki-don.
Profesa ameonesha kuiamini sana video hiyo inayoongozwa na Hefemi, ambayo tangu awali alisema itakuwa katika kiwango cha kimataifa.

“Day one. .. Madirector na maproducer wetu tukiwawezesha WANAWEZA , Asante Mungu. .. #Hatuachii Gap #Nakung'ata mchana kweupeee kama MBU wa DENGU #puna Nikupune #BACK2BACK MUZIK #STRICKLY HIPHOP #TheMastermind of the GAME #Nilimshawishi baba yako akuruhusu Uimbe. ..UNABISHA???” Ameandika Profesa kwenye picha alizoshare Instagram.

"#TATUCHAFU video. ...#MGodi unaotembea kwenye HIP HOP GAME #puna nikupune #Hatuachi gap tena mpaka waombe POOH #MWANALIZOMBE #Video directed by @hefemi Three Locations to GO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni