Jumla ya Mara Iliyotazamwa

20 Ago 2014

NEW UPDATES: BILIONEA LAKE OIL AJISALIMISHA POLISI


Aliyekuwa mfanyakazi wa Bilionea Lake Oil, Ally Edna Awadh aliyejeruhiwa na boss wake.
BILIONEA mmiliki wa kampuni ya usafirishaji na usambazaji wa mafuta Lake Oil, Ally Edna Awadh, aliyekuwa akitafutwa na Polisi kwa kosa la kushambulia na kujeruhi, hatimaye amejitokeza na kujisalimisha ofisi ya upelelezi Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. 

Chanzo chetu cha kuaminika kimesema kuwa mara baada ya kujisalimisha, tajiri huyo alihojiwa na maofisa wa polisi kuhusu sakata lake na maelezo yake kunakiliwa. Hata hivyo, haikujulikana mara moja kama aliachiwa kwa dhamana ya masharti gani. 

Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya jinai nchini (DCI)  Kamishna, Issaya Mngulu alithibitisha kujitokeza kwa Awadh ambaye alitafutwa kwa muda mrefu bila mafanikio.
“Kwa sasa jalada la kesi hiyo limeshaandaliwa tayari kwa kulipeleka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP)  na baada ya hapo suala hilo linaweza kupelekwa mahakamani,” alisema Mngulu. 

Bilionea huyo anakabiliwa na tuhuma ya kumnyanyapaa, kumdhulumu, kumtesa, na kumjeruhi mhasibu wake ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na sababu za kiusalama Mei 2, mwaka jana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni