Jumla ya Mara Iliyotazamwa

20 Apr 2015

Tottenham kuwaombea mema Arsenal katika fainali ya FA Cup

Tottenham may want to see Arsene double up.
Ongeza kichwa

 Tottenham sasa wanawaombea Arsenal wawe mabingwa wa FA Cup ile waweze kufuzu kucheza michuano ya ulaya msimu ujao.

Aston Villa wametinga hatua ya fainali ya kumbe la FA Cup ambapo watachuana na Arsenal ambao wanaonekana tayari wananafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani ulaya(ucl) msimu ujao Aston villa walisha jihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya ulaya msimu ujao yani yuropa ligi, lakin kubadilishwa kwa kanuni mwanzoni mwa msimu huu Aston Villa inahitajika wawe mabingwa wa FA Cup iliwaweze kufuzu katika michuano hiyo.
kipindi cha nyuma, kama bingwa wa FA Cup amefuzu kucheza michuano ya mabingwa ulaya(UCL) au yuropa ligi kutokana na nafasi zao katika ligi, mshindi wa pili yani yule aliyepoteza fainali ya FA Cup alikuwa anapewa nafasi ya kucheza yuropa ligi moja kwa moja, baadhi ya vilabu ambavyo vimeshawahi kunufaika na sheria hii ni Southampton(2003), Millwall(2004) na stoke city(2011) hivi karibuni.
Kuanzia msimu wa 2015-16 UEFA yuropa ligi haitaruhusu washindi wa pili wa FA Cup kufuzu katika michuano hiyo, hivyo basi Aton Villa wanahitajika kumfunga Arsenal katika fainali ili waweza kukata tiketi ya kushiriki yuropa ligi msimu wa 2015-16.
kama Arsenal watakuwa mabingwa wa FA Cup nafasi ya mshiriki wa yuropa itakwenda kwa timu itakayo maliza nafasi ya saba(7) katika ligi kuu ya nchini uingereza nasio mshindi wa pili wa FA.
hivyo basi Tottenham ambao wapo nafasi ya sita(6) katika ligi kuu nchini Uingereza ambayo inaelekea ukingoni, kama wakimaliza nafasi ya saba (7) hawana budi kuwaombea mahasimu wao wakubwa Arsenal kuwachapa Astoni villa ili wao waweze kufuzu katika michuano hiyo ya ulaya.