Jumla ya Mara Iliyotazamwa

5 Sep 2014

NAIBU KATIBU MKUU UVCCM ZANZIBAR MH. SHAKA HAMDU AFANYA MKUTANO CHAKE CHAKE

Mkutano wa hadhara wa vijana wa mikoa miwili ya pemba umemalizika jioni hii ambao ulihubiwa na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar katika viwanja vya Gombani ya kale Chake Chake Pemba.







Commander-in-Chief Uhuru Kenyatta Acts The Part… Wears Army Uniform (PHOTOS)

The president is making a name for himself for being one of the most easy going Head of State.
Every now and then he is seen doing something that is not typical of a president. From dancing with kids, having lunch at a simple hotel..you get the point..he is just an easy going guy.
On Friday morning he was dressed in full military gear as he went to the Validation of Kenya’s pledged forces at Archers Post in Samburu and he was looking sharp. President Moi and Mzee Kenyatta only wore ceremonial uniforms. Kibaki was never seen in any.
Uganda’s Yoweri Museveni and Rwanda’s Paul Kagame however regularly wear army uniforms, perhaps because they were army commanders themselves.
Here are the photos
uhuru1
uhuru2
uhuru3
uhuru4

JENGO LA ZAMANI LA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA YAANZA KUBOMOLEWA


Alama ya Nguvu ya Kijana kwa Taifa

jengo la kihistoria la UVCCM limeanza kubomolewa kupisha ujenzi mwingine wa jengo la vijana
.
HONGERENI SANA VIONGOZI WAKUU WA UVCCM KWA JUHUDI NA HATIMAE YAMEANZA KUTIMIA.

ni akili ya kawaida sana kama mzee Sabodo aliwauliza wale watani zetu niwasaidie nini,,,,kumwambia tu "mzee tunakiwanja bunju tujengee ata jengo la makao makuu ya BAVICHA,,," ni akili tu ya kawaida sana ,,,,LAKINI DUU
WATU WANAPENDA CASH,,,WASHAIMALIZA,,,babu na wenzake

HAYA YANATAKA KUFIKIRI

TWENDENI PAMOJA UVCCM
UMOJA NI USHINDI


MSICHANA ALAZIMISHWA KUFUNGA HARUSI NA MBWA: SOMA HAPA ===>


Msichana wa miaka 18, raia wa India aliyetajwa kwa jina la Mangli Munda amefunga ndoa na mbwa baada ya kulazimishwa na wazazi wake kufanya hivyo kwa imani kuwa atafukuza roho za kishetani na mikosi inayomsonga.

Mbwa huyo alitafutwa na baba mzazi wa mrembo huyo na kufanyika sherehe kubwa ikiwa na vitendo vyote vinavyofanywa na ya bibi harusi na bwana harusi kwa taratibu zao za ndoa.

Kwa mujibu wa Yahoo News, msichana huyo hakuwa na furaha kabisa na alieleza wazi jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho, “Siifurahii kabisa hii ndoa.”

“Tulilazimika kutumia pesa nyingi kwa ajili ya hii ndoa. Hiyo ndiyo njia pekee tunayoweza kufanya kuondoa mikosi aliyonayo na kufanya tendo jema kwa ajili ya kijiji chetu.” Amekaririwa mama yake Munda.

HATARI SANA: NISHA WA BONGO MOVIE AZUA TAHARUKI HEKALU LA FREEMASON DAR!

STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha', Jumanne iliyopita alijikuta akizua taharuki kufuatia kuegesha gari lake nje ya Hekalu la Freemason lililopo nyuma ya Hyatt Regency Dar es Salaam The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam.
Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Taharuki hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason. 

Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo. 

Chanzo chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi huonekana wakiingia na kutoka.
Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.
Kufuatia taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi. 

“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na  kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha. 

Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki. 

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye.

KAJALA NITOE GEREZANI

Stori: Sifael Paul



ANA hoja? Siku chache baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’, mumewe Faraji Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani.
Kajala na mumewe wakiwa mahakamani.
KWANI ILIKUWAJE?
Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo.
UTAJIRI WA GHAFLA
Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla.
HOJA YA MSINGI
Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa.
GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.
Akizungumza kwa huruma, Faraji alisema habari za Kajala kuwa na utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.
Kajala na mumewe siku ya ndoa.
Jamaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time (kipindi cha matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za wikiendi.
Kwa mujibu wa mtu wetu huyo, Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke yeye ni mke wangu. Nimemsaidia kwa mengi, asiniache nateseka huku yeye anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo.
“Bado ni mke wangu, bado nampenda sana. Nilisikia alishavua pete ya ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale. Kama kweli Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu yote. Kama nilivyoahidi kanisani, nitampenda na kumtunza hadi kifo kitutenganishe.”
Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma, azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya kurejesha fedha hizo.Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili kufanikisha jambo hilo.
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’.
INAWEZEKANA?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanasheria wenye uzoefu na kesi za mastaa aliyeomba hifadhi ya jina alisema kwamba jambo hilo linawezekana endapo mteja (mume wa Kajala) ataomba kesi yake ifanyiwe ‘reference’ (mapitio).
“Unajua haya ni mambo ya kisheria, kwa mtu wa kawaida anaweza asiyaelewe kirahisi lakini uwezekano upo bila hata kukata rufaa.“Faraji alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Dar). Kitakachofanyika ni kwamba kama akitaka kesi yake itafanyiwa reference kwenye mahakama ya juu.
“Baada ya hapo Faraji au wakili wake anaweza kuomba kulipa faini badala ya kifungo kwa sababu hukumu ilisema kifungo cha miaka saba au faini ya hiyo shilingi milioni 200.
“Kama kweli Kajala ana hiyo fedha si mbaya akafanya hizo process (taratibu), akamtoa mumewe,” alisema ‘loya’ huyo.
KAJALA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa data hizo, Jumatano iliyopita Ijumaa lilimtafuta Kajala ambaye simu yake haikuwa hewani kila ilipopigwa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo lakini kwenye makabrasha kulikuwa na maelezo yake juu ya mumewe alipohojiwa siku kadhaa zilizopita.
Kwa mujibu wa Kajala, Faraja bado ni mumewe na huwa anakwenda gerezani kumuona kila wikiendi na anatamani awe huru ili waendelee na maisha kwani hawakuwa wamefaidi penzi lao, hata mtoto walikuwa hawajapata.
MARAFIKI WANASEMAJE?
Marafiki wa wanandoa hao waliozungumza na Ijumaa walisema kwamba kama kweli Kajala ana nia hiyo, basi afanye hiv yo kwani itakuwa thawabu kubwa kwake kama alivyofanyiwa na Wema aliyemnusuru kifungo cha miaka mitano jela.

3 Sep 2014

UVCCM IRINGA YAENDELEA KUTHAMINI MICHEZO

IHEMI IRINGA OYEE!!!
Vijana wa CCM wakiwa katika kazi za chama.Wanatengeneza viwanja vya michezo kwa ajili ya vijana wote.
Michezo ni afya,michezo ni ajira.











Mambo Yanayokera Wafanyayo Wanaume Wakiwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi


Kutokubali majukumu , mwanaume umeamua kuwa na mpenzi kuwa responsible na take care of your famili kama ukibahatika kupata mtoto. kwa wadada ukiona mwanaume hayupo responsible ukiwa nae jua hadi kitandani ni mvivu wa kutupa ndio wa kwanza kulalama mmh ujui kukata kiuno. 



Kukiss ujui akilalamika hivyo kaa kimya uone kama anaweza kazi..... utasikia wanawake wanachuna tutaachaje kuchuna wakati kutoa kwa hiyari amtaki mjifunze.

Kujinunisha hovyo hovyo hivi mwanaume unasusa ili iweje ... he he susa wenzio wala.

Kuwa mchoyo.. unakuta mwanaume ni mchoyo kiasi kwamba hata kuhudumiana ni tatizo...
mwanume pesa yako vitu vyako ni tatizo sasa maana ya mimi kuwa mpenzio au mwili mmoja ni ipi kama unaniwekea demacation kwenye vitu vyako... yani hawa hadi kutoa mawazo ni kazi anaona utafaidi...

Mwanume mbahili yani hadi anaumwa au unaumwa kutoa hela ya kutosheleza matibabu hato ... yani sasa huyu wimbo wake wa kila siku utasikia sina hela.. hivi kutokuwa na hela ni sifa au ni uvivu basi tuone unafanya jambo la maana upuuzi mtupu

Mwanume kuendekeza pombe na marafiki yani unatoa kipao mbele rafiki zako kuliko mpenzio ukiona hivyo ujue huna future nzuri.... baadhi ya maandiko yanasema "ajifanyie rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe though rafiki anweza kuwa kama ndugu" tafakari.

Wivu uliopitiliza hapa wengi ni 25 na 30 sana hawa ndio tatizo utasikia baby tuma picha ... tuma picha unatuma bado tena tuma picha ... hivi niwaulize mnatengenezea movie hizo picha ni nini tatizo?...

Jionee Harusi ya kipekee iliyofanyikia ndani ya maji……!!!


Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding …Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.
Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
‘Mtindo tofauti wa picha’
”Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, ” asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
“maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ”
Tina Liu mmiliki wa duka la Mr Wedding
Hawa ni wateja wake, Lin Enxiao na He Huan.
Ndoa yao haijawa tayari kwani wataoana mwaka ujao, lakini wapenzi wengi wachina wanasema wameamua kujipiga picha zao za harusi mapema ili wasipate tatizo lolote.
”Marafiki wetu wengi walijipiga picha katika eneo kavu,” asema YY. “sisi tulitaka kitu tofauti. ”
Watu wanapofikiria kuhusu picha za harusi, wao hutaka kujipiga sehemu kavu kuliko kuta nyeupe au nyasi, ” asema Lamea.
“sisi tunahisi vyema kubadili mtindo huo.”
Sio mara ya kwanza kuona watu wakipigwa picha wakiwa ndani ya maji wala China sio nchi ya kwanza kuanzisha mtindo huu, ila China imeanza kuitumia kwa njia ambayo imewapendeza wengi.
‘Vipodozi visivyoharibiwa na maji’
Kuna studio nyingi za picha zinazotoa huduma hii nchini China, soko lina ushindani mkali lakini baadhi ya wafanyabiashara hawana maadili ya kazi.
”Baadhi ya wafanyabiashara wana uelewa wa kazi na ni wabunifu lakini huwa hawadumu kwa sababu wanakosa maadili ya kazi. ”
Duka hili la Mr Wedding lina wabunifu wengi ambao huwa wanawapendekezea maharusi namna ya kupigia picha , wakitumia muda mwingi kuwapodoa na kuwapamba nywele maharusi.
“tunapendekeza bibi harusi akiwa ndani ya maji avalie gauni nyeupe na ndefu. Na sisi hutumia vipodozi ambavyo haviwezi kuharibiwa na maji. ”
Kisha maharusi hawa wanatembezwa na kuingizwa ndani ya tenki ya maji ambako wanapigiwa picha.
Tenki hiyo huwa na maji ya vuguvugu na mtu wa kuwasidia maharusi pia huwa ndani ya tenki hiyo ambamo wanapigiwa picha.
Tina alianza kazi hii mwaka 2003 wakati huo akipiga picha tu za kawaida za harusi kabla ya kuanza kuwapiga picha watu wakiwa ndani ya maji.
Kila biashara zina changamoto zake. Kwa Tina lazima awe na maarifa ya utenda kazi ili kazi yake iweze kunawiri.

VIVU WAKO NI SABABU YA MWENZIO KUCHEPUKA NJE



Wakati mwanamke anapobana ‘staftahi’ kwa mwenzake, huhesabika ni mchoyo! Kwa mwanaume yeye huonekana ni goigoi. Kwamba mambo hayawezi ndiyo maana hatekelezi shughuli.

Kuna watu wengi ambao hupenda kujisifu kuwa wao hutoa unyumba kwa kibaba, yaani huwabania wenzi wao, ila kwa mitazamo yao hujiona wako sahihi kabisa, tabia yanamna hii wanayo sana wenzetu akina mama na akina dada. japo pia kwa upande mwingine wapo wanaume ambaonao hawawezi kutekeleza mahitaji ya wapenzi wao.



Ataambiwa ana tatizo la zile nguvu zetu! Mwanamke anaweza kujisifu hata kwa wenzake. Akiwa kwenye vikao vya kusukana au katika soga nyingine, atajimwagia sifa tele kwamba yeye inaweza kupita miezi bila kuingia uwanjani na mwenzi wake.

Hili, linawafanya wanaume wengi wateseke na matokeo yake hutafuta tiba mbadala. Mwanaume hawezi kujisifu kwa marafiki zake kuwa yeye huwa akisumbuliwa na mwenzi wake, humpa mgongo! Ni wazi akisema hivyo atachekwa.

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.

MAKALIO FEKI YAMUUMBUA LIVE STAA HUYU MJINI MCHANA KWEUPE!


Oops! wahenga walisema ajali haina kinga!!
Blac Chyna ni rafiki yake kipenzi Kim Kardashian na pia ni mama mtoto wa rapper Tyga. Mdada huyo ambaye zamani alikuwa ni stripper, amekuwa ni gumzo kwa muda mrefu kutokana na makalio yake ambayo watu wengi wanasema ni ya bandia yaani fake.
Lakini mrembo humbo ambaye kwa sasa ni model, alikanusha uvumi huo na kusema makalio yake ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Yaliyojiri hivi karibuni, ni kwamba makalio hayo yalianza kuporomoka taratibu wakati anatembea na alipigwa picha akijaribu kuyafunika na sweta.

Inasemekana dada huyo alionekana akikimbilia kwa dotka kwa ajili ya marekebisho ya fasta.....majanga!! Watu wanasema makalio ya Kim yanaweza kuwa bandia pia―Samaki mmoja akioza, wote wameoza heheh!

UNDANI NA PICHA ZAIDI JUU YA KUUNGUA KWA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA

JUMBA lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya
washiriki wa shindano la Big Brother Africa
(BBA ) 2014 limeteketea kwa moto jana eneo la
Sesani Studios jijini Johannesburg nchini
Afrika Kusini.

Kuteketea kwa jumba hilo kumesababisha
uzinduzi wa shindano hilo kwa mwaka huu
kusogezwa mbele tofauti na awali ambapo
ulitarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya
Septemba 7, mwaka huu .
Katika taarifa iliyotolewa na waandaaji wa
shindano hilo, M- Net na Endemol ni kwamba
katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na
chanzo cha moto huo bado hakijafahamika
huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo
chake.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kwa sasa
linatafutwa jumba lingine litakapoendeshwa
shindano hilo linalochukua siku 91 .

KICHENI PATI YA LUCY KOMBA MSHANGAO!



Stori: Imelda Mtema
NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.

Staa wa filamu Bongo, Lucy Komba.
Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria.
Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni.
Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.

Akiwa kwenye usafiri wa baiskeri ya matairi matatu maarufu kama ‘Guta’.GPL(P.T)
Kama hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.
“Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.
Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.

Akiingia ukumbini kwa mbwembwe.
Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.

1 Sep 2014

CCM YAIBOMOA NGOME YA CHADEMA NYOLOLO

Alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Rubeni Mwagala,
akimwaga manyanga katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika
Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Aliyekuwa Afisa Habari Msaidizi Wilaya ya Mufindi Desius Nyoni
akionyesha kadi mpya katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika
katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA FRIDAY
SIMBAYA)

Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada
kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA)

Aliyekuwa Afisa Habari Msaidizi Wilaya ya Mufindi Desius Nyoni
akionyesha kadi mpya katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika
katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA FRIDAY
SIMBAYA)


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
akitoa kadi ya CCM

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
akitoa kadi ya CCM

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga KATIKATI
Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada
kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA)

 Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada
kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA)


NA FRIDAY SIMBAYA, MUFINDI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi kimeisambaratisha ngome ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kufanikiwa
kuwahamisha viongozi na wanachama 170 wa CHADEMA akiwamo Afisa Habari
wa Wilaya hiyo, Rubeni Mwagala.
Viongozi na wanachama hao wa CHADEMA wakiongozwa na Rubeni Mwagala,
ambaye alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi,
walitangaza rasmi kuachana na chama hicho katika mkutano wa hadhara wa
CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alizindua shina la
wakeleketwa CCM Nyololo na baadaye aliwakabidhi kadi za uanachama wa
wanachama wapya katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya
wakazi wa kijiji hicho.
Viongozi wengine wa Chadema waliohamia CCM ni pamoja na  afisa habari
msaidizi wa wilaya ya mufindi, Desius Nyoni na Afisa habari
muamasishaji wa wilaya hiyo Meja Mfilinge.
Wana CHADEMA hao waliohamia CCM walikiponda vikali chama hicho kimejaa
ubabe,  ukabila na kwa kufanya siasa za vurugu hapa nchini.
Kwa upande wake afisa habari huyo wa CHADEMA, Rubeni Mwagala
aliwaomba radhi wananchi wa Nyololo kwa polisi kuwapiga mabomu tarehe
2 Septemba mwaka 2012 na kuplekea kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa
kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi katika Kijiji
cha Nyololo wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa akiwa kama afisa habari wa chadema wilaya ya mufindi
ndiye aliyeratibu kufanyika mkutano na kupelekea mwandishi wa habari
wa Chanel Ten Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti chama cha waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC), Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za
polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Naye Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwasihi wananchi
waKijiji cha Nyololo na kwengineko wasibeze hatua ya maendeleo
yaliyofanywa na chama tawala.
Alitoa mifano hiyo ya maendeleo katibu huyo alisema wakati nchi hii
inapata uhuru kutoka kwa wakoloni nchi ilikuwa barabara za lami
kilometa 300 lakini mpaka sasa kuna barabara  za lami zenye urefu
kilometa 17,800.
Alisema nchi wakati huo ilikuwa na vyuo vikuu vichache lakini leo hii
ina jumla ya vyuo vikuu 34 na kuongeza kuwa hapo zamani kulikuwa na
madakatari bingwa wachache lakini leo hii kuna madaktari  bingwa 5200.
Aliwaasa pia wananchi kulinda amani iliyopo nchini kama mboni ya jicho
na kuongeza kuwa ni heri kula dagaa kwenye nyumba yenye amani kuliko
kula minofu ya sangara kwenye nyumba ya vita.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi komradi Miraji Mtaturu
alisema wakati umefika sasa wananchi wa Mufindi kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za
hasira baina ya CHADEMA na kisha kuisambaratisha kabisa ngome hiyo
kuwachagua viongozi wa kwa maendeleo yao.
Mwisho