Jumla ya Mara Iliyotazamwa

1 Sep 2014

[EXCLUSIVE] MAMBO 6 MUHIMU USIYOYAFAHAMU KUHUSU LINAH NA HIT SINGLE YA OLE THEMBA!


Nafasi yake nyingine kubwa ya kuzungumziwa toka ameanza muziki ni hii aliyoipata baada ya kufanya wimbo wa ‘Ole Themba’ na kundi maarufu la Uhuru South Africa.

Ni kolabo ambayo mpaka August 31 2014 usiku video yake YouTube ilikua imebakiza sio chini ya views elfu mbili ili kufikisha views laki moja za wote walioitazama toka iweke July 2014.

Yafuatayo ni mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’.

1. Video hii ya ‘Ole Themba’ imeanza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV Africa ikiwemo MTV Base pamoja na TV ya Ufaransa ya TRACE Urban ambao tayari wameshamtumia Linah mkataba wa makubaliano.

2. Wakati aliposafiri kwenda Afrika Kusini kuirekodi hii single na Uhuru, alikaa kwa mwezi mmoja bila kufanya chochote mpaka kufikia kukata tamaa manake Uhuru kama walimuwekea ‘pozi’ japokua Linah alikua na pesa mkononi tena milioni za Tanzania kwa ajili ya kulipia kurekodi nao hiyo single kama makubaliano yalivyokuwa.

3. Linah anasema Producer wa Uhuru aliwatajia hela nyingi kurekodi hiyo kolabo akidhani watashindwa kuilipia lakini haikua hivyo, mwanzoni aliwawekea pozi kwa kuagiza atumiwe link za video za Linah YouTube ili ajue uwezo wake lakini hakuwahi kuzitazama. 
4. Producer huyu alikua akipigiwa simu mara nyingi lakini hakuwa anapokea na hata msg anaweza kujibu au kutojibu ambapo linah anasema ‘ilikua ngumu sana mwanzoni lakini baada tu ya kuingia studio kuweka voco ya kwanza nikapata na kolabo hapohapo, yani walikubali uwezo wangu’

5. Baada ya Uhuru kuona single ya ‘Ole Themba’ imeanza kuwa kubwa kwa kufanya vizuri kwenye Radio na TV kulitokea kama kutokuelewana kidogo kwa kuona Linah anaanza kupata hela. 


6. ‘Waliitengeneza kama na wao wana haki na wimbo wenyewe lakini uzuri ni kwamba tulishasaini mkataba mwanzoni kuwa wimbo wametuuzia ni mali yetu na wala hawana haki yoyote, alietunga melody alisaini na tumemlipa so hausiki tena, tulimlipa kila mtu na kazi yake…. namshukuru Mungu iliisha vizuri’- Linah

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni