Jumla ya Mara Iliyotazamwa

3 Sep 2014

VIVU WAKO NI SABABU YA MWENZIO KUCHEPUKA NJE



Wakati mwanamke anapobana ‘staftahi’ kwa mwenzake, huhesabika ni mchoyo! Kwa mwanaume yeye huonekana ni goigoi. Kwamba mambo hayawezi ndiyo maana hatekelezi shughuli.

Kuna watu wengi ambao hupenda kujisifu kuwa wao hutoa unyumba kwa kibaba, yaani huwabania wenzi wao, ila kwa mitazamo yao hujiona wako sahihi kabisa, tabia yanamna hii wanayo sana wenzetu akina mama na akina dada. japo pia kwa upande mwingine wapo wanaume ambaonao hawawezi kutekeleza mahitaji ya wapenzi wao.



Ataambiwa ana tatizo la zile nguvu zetu! Mwanamke anaweza kujisifu hata kwa wenzake. Akiwa kwenye vikao vya kusukana au katika soga nyingine, atajimwagia sifa tele kwamba yeye inaweza kupita miezi bila kuingia uwanjani na mwenzi wake.

Hili, linawafanya wanaume wengi wateseke na matokeo yake hutafuta tiba mbadala. Mwanaume hawezi kujisifu kwa marafiki zake kuwa yeye huwa akisumbuliwa na mwenzi wake, humpa mgongo! Ni wazi akisema hivyo atachekwa.

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni