Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo
sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini
China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo
kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya
imeanza kufanyika hapa.Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding …Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.
Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
‘Mtindo tofauti wa picha’
”Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, ” asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
“maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ”
Tina Liu mmiliki wa duka la Mr Wedding
Ndoa yao haijawa tayari kwani wataoana mwaka ujao, lakini wapenzi wengi wachina wanasema wameamua kujipiga picha zao za harusi mapema ili wasipate tatizo lolote.
”Marafiki wetu wengi walijipiga picha katika eneo kavu,” asema YY. “sisi tulitaka kitu tofauti. ”
Watu wanapofikiria kuhusu picha za harusi, wao hutaka kujipiga sehemu kavu kuliko kuta nyeupe au nyasi, ” asema Lamea.
“sisi tunahisi vyema kubadili mtindo huo.”
‘Vipodozi visivyoharibiwa na maji’
Kuna studio nyingi za picha zinazotoa huduma hii nchini China, soko lina ushindani mkali lakini baadhi ya wafanyabiashara hawana maadili ya kazi.
”Baadhi ya wafanyabiashara wana uelewa wa kazi na ni wabunifu lakini huwa hawadumu kwa sababu wanakosa maadili ya kazi. ”
Duka hili la Mr Wedding lina wabunifu wengi ambao huwa wanawapendekezea maharusi namna ya kupigia picha , wakitumia muda mwingi kuwapodoa na kuwapamba nywele maharusi.
“tunapendekeza bibi harusi akiwa ndani ya maji avalie gauni nyeupe na ndefu. Na sisi hutumia vipodozi ambavyo haviwezi kuharibiwa na maji. ”
Tenki hiyo huwa na maji ya vuguvugu na mtu wa kuwasidia maharusi pia huwa ndani ya tenki hiyo ambamo wanapigiwa picha.
Tina alianza kazi hii mwaka 2003 wakati huo akipiga picha tu za kawaida za harusi kabla ya kuanza kuwapiga picha watu wakiwa ndani ya maji.
Kila biashara zina changamoto zake. Kwa Tina lazima awe na maarifa ya utenda kazi ili kazi yake iweze kunawiri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni