Jumla ya Mara Iliyotazamwa

1 Sep 2014

CCM YAIBOMOA NGOME YA CHADEMA NYOLOLO

Alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Rubeni Mwagala,
akimwaga manyanga katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika
Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Aliyekuwa Afisa Habari Msaidizi Wilaya ya Mufindi Desius Nyoni
akionyesha kadi mpya katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika
katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA FRIDAY
SIMBAYA)

Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada
kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA)

Aliyekuwa Afisa Habari Msaidizi Wilaya ya Mufindi Desius Nyoni
akionyesha kadi mpya katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika
katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA FRIDAY
SIMBAYA)


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
akitoa kadi ya CCM

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
akitoa kadi ya CCM

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga KATIKATI
Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada
kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA)

 Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada
kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.  (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA)


NA FRIDAY SIMBAYA, MUFINDI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi kimeisambaratisha ngome ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kufanikiwa
kuwahamisha viongozi na wanachama 170 wa CHADEMA akiwamo Afisa Habari
wa Wilaya hiyo, Rubeni Mwagala.
Viongozi na wanachama hao wa CHADEMA wakiongozwa na Rubeni Mwagala,
ambaye alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi,
walitangaza rasmi kuachana na chama hicho katika mkutano wa hadhara wa
CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alizindua shina la
wakeleketwa CCM Nyololo na baadaye aliwakabidhi kadi za uanachama wa
wanachama wapya katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya
wakazi wa kijiji hicho.
Viongozi wengine wa Chadema waliohamia CCM ni pamoja na  afisa habari
msaidizi wa wilaya ya mufindi, Desius Nyoni na Afisa habari
muamasishaji wa wilaya hiyo Meja Mfilinge.
Wana CHADEMA hao waliohamia CCM walikiponda vikali chama hicho kimejaa
ubabe,  ukabila na kwa kufanya siasa za vurugu hapa nchini.
Kwa upande wake afisa habari huyo wa CHADEMA, Rubeni Mwagala
aliwaomba radhi wananchi wa Nyololo kwa polisi kuwapiga mabomu tarehe
2 Septemba mwaka 2012 na kuplekea kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa
kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi katika Kijiji
cha Nyololo wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa akiwa kama afisa habari wa chadema wilaya ya mufindi
ndiye aliyeratibu kufanyika mkutano na kupelekea mwandishi wa habari
wa Chanel Ten Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti chama cha waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC), Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za
polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Naye Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwasihi wananchi
waKijiji cha Nyololo na kwengineko wasibeze hatua ya maendeleo
yaliyofanywa na chama tawala.
Alitoa mifano hiyo ya maendeleo katibu huyo alisema wakati nchi hii
inapata uhuru kutoka kwa wakoloni nchi ilikuwa barabara za lami
kilometa 300 lakini mpaka sasa kuna barabara  za lami zenye urefu
kilometa 17,800.
Alisema nchi wakati huo ilikuwa na vyuo vikuu vichache lakini leo hii
ina jumla ya vyuo vikuu 34 na kuongeza kuwa hapo zamani kulikuwa na
madakatari bingwa wachache lakini leo hii kuna madaktari  bingwa 5200.
Aliwaasa pia wananchi kulinda amani iliyopo nchini kama mboni ya jicho
na kuongeza kuwa ni heri kula dagaa kwenye nyumba yenye amani kuliko
kula minofu ya sangara kwenye nyumba ya vita.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi komradi Miraji Mtaturu
alisema wakati umefika sasa wananchi wa Mufindi kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za
hasira baina ya CHADEMA na kisha kuisambaratisha kabisa ngome hiyo
kuwachagua viongozi wa kwa maendeleo yao.
Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni