Jumla ya Mara Iliyotazamwa
1 Sep 2014
Exclusive : Diamond alivyotaka kupigwa na mashabiki ujerumani, aokolewa na polisi…
Kama isingekuwa polisi wa Ujerumani leo tungekuwa tunaongea habari nyingine kwakuwa Diamond Platnumz aliponea chupuchupu kushambuliwa na mashabiki wenye hasira jijini Stuttgart nchini humo baada ya kuingia ukumbini saa 10 Alfajiri wakati mashabiki hao walikuwa wakimsubiri tangaa saa 4 usiku.
Uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye ukumbi ambao Diamond alikuwa anatarajia kutumbuiza jijini Stuttgart
Show hiyo ilikuwa ifanyike usiku wa kuamkia jana.
Katika tukio hilo lililoandikwa na vyombo vya habari vya nchini Ujerumani, promota wa show hiyo ambaye ni Mnaijeria alikimbia eneo la tukio na DJ wa show kupewa kipondo cha paka mwizi.
Story kutoka Ujerumani inasema:
Majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya mashabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show. Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi kwa Euro 25 kama kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo Diamond alipopelekwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake. Kilichowakera zaid mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hospitalini kwa sasa.
Polisi wakiwa nje ya ukumbi
Moja wa Djs hao alipoteza Laptop yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali. Mashabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani mashabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashtaka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Kupitia Instagram Diamond alidai kusikitishwa na tukio hilo.
Kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kwa wingi kutusupport vijana wao, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi….
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni