washiriki wa shindano la Big Brother Africa
(BBA ) 2014 limeteketea kwa moto jana eneo la
Sesani Studios jijini Johannesburg nchini
Afrika Kusini.
(BBA ) 2014 limeteketea kwa moto jana eneo la
Sesani Studios jijini Johannesburg nchini
Afrika Kusini.
Kuteketea kwa jumba hilo kumesababisha
uzinduzi wa shindano hilo kwa mwaka huu
kusogezwa mbele tofauti na awali ambapo
ulitarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya
Septemba 7, mwaka huu .
Katika taarifa iliyotolewa na waandaaji wa
shindano hilo, M- Net na Endemol ni kwamba
katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na
chanzo cha moto huo bado hakijafahamika
huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo
chake.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kwa sasa
linatafutwa jumba lingine litakapoendeshwa
shindano hilo linalochukua siku 91 .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni