Na Mathias Canal-Iringa
|
Mwanafunzi Vema Mtati wa chuo cha unesi Chimala wilayani
Mbarali mkoani Mbeya akamatwa na polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za
mauwaji ya mtoto wa siku moja aliyejifungua salama.
Tukio hilo la kinyama limetokea leo saa 12 jioni katika
eneo la Kijiweni kata ya Mvinjeni Manispaa ya Iringa kutokana na baadhi
ya majirani kufichua siri hiyo nzito ya kuwepo kwa jaribio za binti huyo
kufanya mauwaji hayo.
Mmoja kati ya majirani aliueleza kuwa binti huyo mwanafunzi
akiwa na mimba ya miezi tisa alifika katika nyumba hiyo kwa rafiki yake
ambae ni mfanyakazi wa bar mmoja eneo la vibanda vya CCM mjini Iringa
aliyefahamika kwa jina la Joys siku kama tano kabla ya usiku wa jana
kujifungua salama katika chumba hicho.
Shuhuda huyo alidai kuwa mapema asubuhi ya leo
walisikia sauti ya mtoto mchanga akilia huku sauti ya radio
ikipandishwa kupoteza sauti ya mtoto huyo ili wapangaji wengine
wasijue suala hilo.
Hivyo kutokana na hali hiyo ndipo waliamua kufika ofisi
za mtandao huu kufichua siri hiyo kwa maombi ya kutotajwa popote jina
la shuhuda huyo.
" Mimi ni raia mwema na mwanamke mwenye uchungu
nimekuja kwako huku nikijua hutatoa siri hii ...katika nyumba ambao
naishi kuna mwanafunzi amejifungua mtoto jana usiku na kwa sasa
amejifungia ndani na mwenye chumba anaitwa Joys anafanya kazi vibanda
vya CCM sasa lengo la kujificha nafikiri ni kutaka kufanya jaribio
la kuua mtoto huyo sasa naomba usaidie kuokoa maisha ya mtoto huyo
unatusaidiaje na sisi kwenda polisi tunaogopa ushahidi"
Kutokana na maelezo hayo yasio na chembe ya uongo
mtandao huu ulipiga simu kwa OCD Iringa Bw Pyuza na bila kuchelewa
kikosi kazi akiwemo askari wa dawati la jinsia kilifika katika ofisi
za mtandao huu wa matukiodaima na safari ya kufuatilia suala hilo
ilipoanza kwa kumkamata mwenyeji wa mwanafunzi huyo ambae ni mmiliki wa
chumba kisha kupokonywa simu yake ili asifanye mawasiliano nyumbani
na baada ya hapo kwenda katika nyumba husika .
Hata hivyo ukweli wa jambo ulianza kujionyesha baada ya
kufika katika chumba hicho na kukuta mlango umefungwa kwa ndani na
baada ya mwenye chumba kugonga ndani mwanafunzi huyo aliigiza kuwa
alikuwa akifanya usafi ila baada ya kuhojiwa na polisi alidai kuwa kwa
sasa ana mtoto mmoja ambae yupo kijijini Magulilwa wilaya ya Iringa .
Uchunguzi wa kipolisi ulianza na kikosi hicho kwa maswali
ya kiuchunguzi na ndipo alipokiri kuwa anamtoto mwingine ambae
amejifungua usiku wa leo na amemhifadhi katika mfuko wa rambo ndani
chini ya kitanda .
Alipotakiwa kumtoa alifanya hivyo na polisi na mmiliki
wa mtandao huu kushindwa kujizuia kuangua kilio kutokana na kile
walichokiona kutoamini .
Mtoto huyo alikutwa amekufa huku akiwa amefungwa na nguo
nyingi pamoja na kumwagiwa vumbi ya mkaa na chumvi ili asitoe harufu
na kufungwa vizuri katika mfuko wa rambo mweusi kisha kuwekwa katika
mfuko mkubwa wa salfeti tayari kwa kuvuta subiri ya kwenda kumtupa
mtoto huyo porini .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni