Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper.
Kwa mujibu wa rafiki mmoja wa karibu na Wolper (jina lipo),
anamshangaa sana shoga yake huyo kwani amekuwa akibadili namba za simu
kwa mwaka mmoja hata mara saba.“Unajua kwa maisha ya sasa, simu ikipotea mtu unairinyuu laini yako ileile, maana ndiyo inayojulikana na wadau. Lakini yule mwenzetu siyo. Nimeshamsevu kwenye simu yangu kwa majina ya Wolper, Wolper Tena, Wolper Nyingine, Wolper Nyingine Kabisa na Wolper Hakuna Tena, lakini zote kwa sasa hazipo hewani,”alisema shoga yake huyo huku akicheka Wolper alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi iliyozoeleka, hakupatikana. Jitihadi zilifanyika akaja kupatikana kwenye namba mpya ambapo alisema:
“Mimi nikishapoteza laini naona uvivu kwenda kuirinyuu, ndiyo maana nanunua nyingine.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni