Mwenyekiti UVCCM mkoa
wa Arusha Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi
wa habari juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo
vya habari na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano
huo ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
waliaofikiana kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM
Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi
mabaya ya fedha za umoja huo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu Ally
Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga marufuku Kaimu
Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe na kazi za
UVCCM mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa UCVVM Mkoa wa Arusha Robnson
Meitinyiku na baadhi ya wajumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
wakisikiliza maazimio yaliyopitishwa na wajumbe wakati yalipokuwa
yakisomwa mbele ya waandishi wa habari mjini hapa
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM
Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi katikatika pamoja na wajumbe wenzake
wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande wake alitoa
ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua watendaji
lie linaangalia watendaji wenye sifa.
Sehemu ya mkutano wa waandishi wa habari
na wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kikiendelea leo
katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatulia
maazimio yaliyofikiwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
kilichofanyika leo jioni.Ambapo Baraza hilo liliazimia kuanza kufanyiak
kwa ukaguzi wa mara kwa mara katika ofisi za UVCCM mkoa kwa kila mwezi
kwa ajili ya kdhibiti ubadhilifu.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la
UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini ajenda za kikao hicho,
ambapo Baraza hilo lililaani kitendo cha Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa cha
kufunga ofisi ili Kamati ya Utekelezaji isifanye kikao ambacho
walikubaliana pia kitendo cha kukwepa kuitisha vikao licha ya
kukubaliana na Mwenyekiti kama kanuni inavyotaka na kuuotosha umma
kwamba Kamati ya Utekelezaji ndio iliyofunga ofisi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Robson Meitinyiku
akifuatilia kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha kilichofanyika leo
jijini hapa na kupitia maazimio ya kumtaka Katibu wa CCMM Mkao Mary
Chatanda asiingilie Jumuiya hiyo bali awe mshauri kupitia bvikao vya
jumuiya ambapo yeye ni Mjumbe katika vikao vya Utekelezaji na vya Baraza.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la
UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia maazimio yaliyokuwa yakisomwa mbele ya
wanahabari leo mjini hapa ambapo Baraza hili liliazimia kwamba endao
Katibu wa Mkoa Mary Chatanda atabainika kuwa na ubadhilifu basi
asihamishwe mkoa mwingine na apelekwe mahakamani ili iwe fundisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni