BAADA ya hivi karibuni Katibu wa Bongo Movie Unity, William Mtitu kutangaza kujiuzulu na kuiacha nafasi hiyo wazi, Katibu Msaidizi, Devota Mbaga amefunguka kuwa anajiandaa kushika nafasi na kwamba kujiuzulu kwake hakusaidii chochote kwani wanachama wanahitaji fedha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Devota Mbaga.
Akistorisha na paparazi wetu Devota alisema hatua ya Mtitu kujiuzulu haisaidii kitu, wanachama wanahitaji fedha ambazo wamekula kwani alitangaza kujiuzulu baada ya kuambiwa aweke mezani fedha walizokula.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William J. Mtitu akitabasamu ndani ya studio za Global TV Online.
“Najiandaa kushika wadhifa huo kufuatia Mtitu kuachia nafasi baada ya kuambiwa aweke mezani fedha walizokula, amefanya hivyo, ili aonekane msafi arudishe fedha au aje awaombe msamaha wanachama,” alisema Devota.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni