BAADA ya kuachwa na mpenzi
wake wa siku nyingi Bond, ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mwigizaji wa filamu, Wastara Juma, Aunty Lulu amekubali
yaishe na sasa hana tena kinyongo nao.
Mwigizaji wa filamu Bongo, 'Aunty Lulu'.
“Mimi sina tena kinyongo na Wastara, vile
nilikuwa namfanyia tu vituko, lakini kwa sasa asiniogope wala asiwe na
wasiwasi na mimi, nimeshaachana na Bond japokuwa tulitoka mbali sana na
hakuna wanamke anayemjua kama mimi, siku ya harusi yao nitacheza mpaka
asubuhi,”alisema Aunty Lulu.
Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma akiwa na muigizaji mwenzake 'Bond'.
Msichana huyo aliyepata umaarufu baada ya kutwaa taji la Kimwana
Twanga Pepeta, alitoa kauli hiyo hivi karibuni maeneo ya Kinondoni baada
ya kutakiwa kutoa tamko juu ya uhusiano wa wawili hao, ambao awali
alikuwa akiwatupia madongo na kuwapiga vijembe.Alisema kwa sasa hana kinyongo na Wastara na amebariki uhusiano wao wa kimapenzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni