Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt Natalia Kanem akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya
siku ya kimataifa ya vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM) Kushoto ni Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga na kulia ni Mtaalamu
wa Programu za Vijana kutoka UNFPA, Tausi Hassan.( Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
.Siku ya vijana duniani na ujumbe wa “Vijana na Afya ya Akili”
.Takwimu zinaonyesha nusu ya idadi ya watu nchini ni vijana
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
Kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeahidi kukuza
na kuboresha misingi ya kuwashirikisha vijana katika utekelezaji wa sera
mbalimbali, programu na mikakati ya maendeleo.
Akisoma
hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na
Michezo, Bibi Sihaba Nkinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya vijana
duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bibi Venerose
Mtenga amesema kwamba lengo la kuwashirikisha vijan ni kuhakikisha kuwa
sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi.
“Katika
kutekeleza eneo hili Tanzania inalenga kuweka fursa zitakazowawezesha
vijana kukuza utaalamu na ujuzi utakaowawezesha kufanikiwa katika
kipindi cha mpito kutoka ujana kwenda katika utu mzima,” amesema Bibi
Mtenga.
Amesema
kwamba Tanzania kama sehemu ya dunia inatambua changamoto maalum
zinazowakabili vijana walioko katika mazingira hatarishi pamoja na
umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kikamilifu katika
malengo ya maendeleo.
Bi
Mtenga aliongeza Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vijana
pamoja na wadau wa maendeleo ili kuunga mkono programu za elimu ya afya
kwa vijana walioko ndani na nje ya shule.
Alilisitiza
kwamba Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wataendelea
kuunga mkono taasisi za mafunzo rasmi na zisizo rasmi ili kukuza uwezo
na uelewa miongoni mwao katika masuala ya afya ya akili na mwili kwa
ujumla.
“siku
ya vijana duniani inatambua na kuthamini kuwa kipindi cha ujana
kinaambatana na mabadiliko makubwa na ya haraka na safari ya kutoka
utotoni kufikia utu mzima,”
“Safari
hiyo inaweza kuwa ngumu na yenye changamoto nyingi na hivyo kuhitaji
utulivu na ukomavu wa akili, hapa Tanzania, kwa mujibu wa Sera ya Taifa
ya Maendeleo ya vijana, kijana ni mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka
15 hadi 35,” aliongeza
Amesema
kwamba katika takwimu za kitaifa hapa nchini nusu ya idadi ya watu ni
vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Mgeni
Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi
Venerose Mtenga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani, kushoto kwake, ni Mwakilishi wa UNFPA, Dkt.
Natalia Kanem.
Bibi
Mtenga aliendelea kusema kwamba msisitizo mkubwa unawekwa katika
kuhakikisha vijana wanakuwa na fikra chanya ambazo ni za kimaendeleo na
zinazoleta mabadiliko chanya kwa jamii.
Kwa
Upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem
amesema kwamba siku ya vijana duniani ni nafasi nyingine kwa vijana
kukutana pamoja na kujadiliana matatizo na changamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo.
Amesema
kwamba vijana kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa katika kupambana na changamoto za matumizi ya pombe kupita
kiasi, dawa za kulevya na mimba za utotoni.
“kwa
pamoja serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya
kimataifa wana wajibu wa kushirikiana na vijana katika kuwasaidia
kufikia malengo yao mbalimbali katika harakati za kujiletea maendeleo,”
amesema Dkt. Kanem.
Baadhi
ya timu za mpira wa kikapu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za
sekondari nchini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku
ya kimataifa ya vijana duniani.
Dkt Kanem aliongeza kwamba ni muhimu kwa vijana kutambua kwamba bila
kuwa na afya nzuri ya akili ni vigumu kupiga hatua za kimaendeleo na
kuondokana na umaskini wa kipato.
Amesema
kwamba katika mkutano unaokuja wa viongozi duniani watatumia nafasi
hiyo kuwakumbusha viongozi wa dunia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana kama
taifa la kesho.
Dkt.Kanem
alifafanua umuhimu wa vijana na jamiii kwa ujumla kutumia mitandao ya
kijamii katika kupashana habari za afya ya uzazi na mambo yanayowahusu
vijana kwa ujumla.
Wakati
huo huo, Katika mashindano ya mpira wa kikapu timu zilizoshiriki ni
timu saba kati ya hizo tano ni za wanaume na pili za wasichana.
Kwa
upande wa wasichana mshindi wa kwanza ni Don Bosco Lioness na washindi
wa pili ni Tanzania Prisons Queens na kwa upande wa wavulana, washindi
wa kwanza Lord Baden-Powell Memorial High School, washindi wa pili
Makongo High School, washindi wa tatu ni Kizuka Sekondari school.
Timu
zilizoshiriki ni Tanzania Prisons Queens, Lord Baden-Powell Memorial
High School, Makongo High School, Don Bosco Lioness, Kizuka Sekondari
School, Tabata Segerea na Bahari Beach.
Mgeni
rasmi, Venerose Mtenga akirusha mpira wa kikapu kuzindua rasmi
mashindano ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana wa shule za sekondari
nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mwakilishi
wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem akirusha mpira wa kikapu kuashiria uzinduzi
rasmi wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mgeni Rasmi na Mwakilishi wa UNFPA wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya timu za mpira wa kikapu.
Mgeni
rasmi, Venerose Mtenga akiwa katika picha ya pamoja na timu ya
wasichana ya mpira wa kikapu wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya
vijana duniani.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama (kulia) na Mgeni rasmi, Venerose Mtenga (kushoto) wakimuonyesha
jambo Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem (katikati) mara baada ya
kupata picha za kumbukumbu na timu zilizoshiriki bonanza hilo la mpira
wa kikapu katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mwakilishi
wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem akisalimiana na msanii muziki wa bongo
flava Domokaya (wa pili kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani.
Mtaalam
wa Mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza akipata u-selfie na msanii
wa bongo flava Domokaya wakati wa maadhimisho hayo.
Phillip
Musiba kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akipata
picha na msanii wa muziki wa bongo flava nchini Domokaya.
Timu
za Kizuka sekondari kutoka Morogoro, (Nyeupe) na Makongo Sekondari
(Njano) wakitoana jasho katika mchezo wa ufunguzi wa mpira wa kikapu,
Makongo walishinda vikapu 30 dhidi ya 14 ya Kizuka sekondari kutoka
Morogoro.
Mgeni
Rasmi, Bibi Venerose Mtenga akifafanuliwa jambo kutoka kwa Mshauri wa
vijana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu
duniani (UNNFPA), Bw, John Kalimwabo alipotembelea banda hilo.
Mgeni
Rasmi, Bibi Venerose Mtenga akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Tatu
Mwakifuna na Mwanafunzi wake, Zawadi Salehe wote kutoka KIWOHEDE.
Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mtaalamu wa Programu za Vijana kutoka UNFPA,
Tausi Hassan.
Mgeni
rasmi akipata maelezo kutoka kwenye banda la Tanzania Network Against
Alcohol Abuse kwenye moja la shirika lake la Tanzania Girl Guides
Association, anayetoa maelezo ni Fadhia Khamis Ally na kushoto kwake ni
Shadya Soud Milanzi wasichana hao wanatoka Girl Guides ambacho ni chama
kisicho cha kiserikali na ni chama cha kujitolea, madhumuni yake ni
kuwaendeleza wanawake pamoja na motto wa kike katika maswala ya kijamii
na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.
Mgeni
rasmi, Bibi Venerose Mtenga akimsikiliza kijana kutoka Kituo cha Vijana
UMATI, Temeke, Kassim Abdallah alikuwa akimweleza mgeni rasmi jinsi
wanavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa kutumia vipeperushi na
ushauri nasaha.
Wawakilishi
kutoka Marie Stopes Hospital Tanzania, Bibi Zayana Nuhu na John Basso
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wakimweleza jambo mgeni rasmi jinsi
hospitali hiyo inavyofanya kazi hapa nchini.
Mgeni rasmi akipata picha ya kumbukumbu na mmoja wa wahudumu wa banda la Marie Stopes wakati wa maadhimisho hayo.
Joynes
Ashery kutoka Marie Stopes Hospital Tanzania akifafanua jambo kuhusiana
na masuala ya afya ya uzazi kwa Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) ambao ni wameshiriki kuratibu maadhimisho hayo,
Stella Vuzo.
Mshauri
wa vijana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu
duniani (UNNFPA), Bw, John Kalimwabo akitoa maelezo ya matumizi sahihi
ya Kondomu za kike kwa kutumia kiungo bandia cha mwanamke kwa vijana
waliohudhuria maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani.
Vijana
wakiendelea kumiminika kwenye banda ya UNFPA kupata maelezo mbalimbali
wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani
yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM).
Mratibu
wa uzazi wa mpango kutoka shirika la PSI, Hadija Ameir akitoa elimu ya
uzazi wa mpango kwa vijana wakati wa maadhimisho hayo katika viwanja vya
Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akizungumza na baadhi ya watoto walioshiriki mashindano ya kuchora picha
mbalimbali zikiwemo za kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya
madawa ya kulevya baada ya kuvutiwa na kazi zao.
Mtoto Tarzan Iddy akionyesha picha yake aliyoichora ikizungumzia uvutaji wa Bangi kwa vijana.
Mgeni
rasmi, Bibi Venerose Mtenga na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama wakikagua baadhi ya picha
hizo na maudhui kabla ya kutangaza washindi.
Mgeni
rasmi, Bibi Venerose Mtenga akikabidhi nyenzo za sanaa ya uchoraji
zilizotolewa na UNFPA kwa mtoto Lawrence Dennis wakati wa maadhimisho ya
kimataifa ya siku ya vijana duniani.
Mgeni
ramsi Bibi Venerose Mtenga akimkbidhi mmoja kati ya tatu bora wa
mashindano ya uchoraji Aziza Iddy nyenzo za sanaa ya uchoraji kutoka kwa
zilizotolewa na UNFPA sambamba na ufadhili wa kusomeshwa kulipiwa ada
ya darasa la uchoraji kwa siku tano.
Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akiwavalisha medali timu zilizochukua ubingwa wakati wa maadhimisho hayo.
Mgeni
ramsi Bibi Venerose Mtenga akimkabidhi zawadi Kaimu Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Maluwe kama
shukrani ya kuratibu bonanza la mpira wa kikapu kwa vijana wakati wa
maadhimisho hayo.
Mgeni
ramsi Bibi Venerose Mtenga akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa
kwanza wa bonanza la mpira wa kikapu timu ya Lord Baden-Powell.
Timu ya wasichana ya mpira wa kikapu ya Don Bosco Lioness kwenye picha ya pamoja na Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga.
Timu ya waichana ya Don Bosco Lioness wakijipiga u-selfie baada ya kuibuka kidedea kwenye maadhimisho hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni