RONALDO DE LIMA, KLOSE MAGWIJI WA NYAVU.
Licha ya tofauti za mechi walizocheza na utofauti wa Utaifa wao Ronaldo De Lima pamoja na Miroslav Klose ndio wababe wa kuwatesa makipa katika kombe la dunia.
Ronaldo alishastaafu kucheza soka akiwa ameweka rekodi ya kufunga goli 15 katika fainali mbalimbali za kombe la dunia ambaye alitania kwa kuwaambia Wabrazil wamuombee Klose aumie ili asiweze kumfikia na kumpita rekodi yake aliyoiweka.
Katika fainali za mwaka huu zinazofanyika katika nchi ya Ronaldo ndipo Klose kaifikia rekodi ya Ronaldo na bado mechi zipo za kumfanya ampite kabisa.
REKODI KATI YA KLOSE NA RONALDO KATIKA KOMBE LA DUNIA.
Pamoja na kufanana kwa rekodi hiyo pia timu ya Afrika GHANA imeingia katika rekodi wa wabaya wa makipa hao kwa kuwa timu iliyofungwa katika goli zao za 15.
KLOSE NA RONALDO DHIDI YA GHANA.
Cha ajabu katika fainali zote nne za Miroslav Klose hajabadilisha aina yake ya ushangiliaji pindi anapoinyanyasa timu pinzani kwani upendelea kuruka sarakasi.
USHANGILIAJI WA KLOSE
Swali lililobakia katika vichwa vya watu ni je Miroslav Klose atakuwa mfungaji bora wa kipindi chote katika kombe la dunia na kufanikiwa kumpita Ronaldo De Lima?
Swali ilo ni gumu kulijua kwani hakuna aijuae kesho hivyo ni suala la muda na uzima kusubiri kuona rekodi hiyo kama itavunjwa.
Written by Neligwa Mugitttu (Nellynice Mnyiramba)
Great...
JibuFuta