Jumla ya Mara Iliyotazamwa

22 Jun 2014

WAFUMANIA NYAVU BORA
 Kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo utamu wa kombe la dunia unapozidi kuongezeka na hiyo ni kutokana na kiatu cha dhahabu kugombaniwa na wachezaji mbalimbali bila kujali ukubwa wa timu.
Katika fainali za kombe la dunia la mwaka 2010 kule Afrika Kusini, Thomas Muller ndiyo alikuwa mfungaji bora na bado kwa mwaka huu mpaka sasa yupo katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa na magoli matatu aliyopiga hat trick katika mechi yao dhidi ya Ureno wakipowavurumishia mvua ya mabao manne.
Wachezaji wengine wenye mabao matatu ni Robin Van Persie na Arjen Robben wote wa Uholanzi, Karim Benzema wa Ufaransa pamoja Enner Valencia wa Ecuador.
                                                  WASHAMBULIAJI WANAOONGOZA.
Enner Valencia ndiyo mshambuliaji aliyeshitua watu kutokana na kutofahamika kwake sana ukilinganisha na wafungaji wengine kwani anachezea klabu ya Pachuca katika Liga MX. 
Lakini kama kawaida maswali kwetu hayaishi na tunajiuliza je Thomas Muller atatetea ufungaji bora wa dunia au naye atashindwa kutetea kama Uhispania ilivyoshindwa kutetea kombe na kutolewa kwa aibu.
                                 Imeandikwa na Neligwa Mugittu (Nellynice Mnyiramba).

Maoni 1 :

  1. endelea kutembelea blog yetu kwa ushauri na mapendekezo kwani bado tupo mitamboni kwa maandalizi ya kuilaunch.

    JibuFuta