Msanii wa Bongo Fleva,Afande Sele hali yake imekuwa mbaya baada ya kufiwa na mzazi mwenziye Asha Mohamed’Mama Tunda’.
Msanii
huyo inawezekana akawa ni moja kati ya watu maarufu hapa nchini ambao
wanaongoza kwa kuwataja wenza wao sehemu tofauti tofauti ambapo zaidi ya
miaka 10 amesikika akimtaja wa ubavu wake, mara kwa mara hiyo ni wakati
wakiwa wanaishi pamoja na mama tunda ambaye ni mzazi mwenzake waliyezaa
nae watoto wawili, wa kwanza ni Tunda pamoja na Asante Sanaa. Mama
Tunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, na kabla ya kifo chake
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya malaria pamoja na pumu, mazishi ni
leo saa tisa mchana,hata hivyo clouds fm imezungumza na msanii wa karibu
wa Afande Sele,MC Koba baada ya Afande Sele kushindwa kuzungumza
kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni