Jumla ya Mara Iliyotazamwa

26 Sep 2014

MENINAH AFUNGUKA TENA JUU YA TETESI ZA KUFUNGA NDOA NA MSANII DIAMOND PLATINUMZ


YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada
Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kikizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond.
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
Ilisemekana kwamba baada ya Wema kuzinyaka habari hizo kuwa anataka kunyakuliwa ‘beibi’ wake mbaya zaidi wanataka kufunga ndoa, malkia huyo mkubwa wa sinema Bongo aligeuka mbogo na kuanza kuweka mikakati ya kumteketeza Meninah asiweze kufunga ndoa na Diamond.
Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem.
Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star 
Kuna madai kwamba Meninah aliposikia Wema anamsaka usiku na mchana ili amshikishe adabu, msanii huyo alishtuka kwa kuwa anaujua vizuri ‘mziki’ wa staa huyo.
Diamond
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
VIKAO VYA HARUSI VYAFANYWA
Taarifa ziliendelea kudai kwamba, vikao vya harusi vya chinichini vinaendelea kufanywa huku wahudhuriaji wakiwa ni mdogo wa Diamond ambaye pia ni mwanamuziki, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darlin’ pamoja na baadhi ya ndugu wa upande wa mama Diamond ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa.
POMBE NA STAREHE VYATAJWA
Sababu kubwa inayosemekana Wema kutemwa kuolewa na Diamond ni kutokana na kuendekeza pombe na starehe jambo ambalo Meninah yupo nalo kando na kwamba hivi sasa amekuwa akitimba kwa mama Diamond bila wasiwasi huku akizama jikoni kupika, kupakua na kufanya kazi ndogondogo za ndani ili kuthibitisha kuwa yeye ni mama bora.
DIAMOND AMTOA MACHOZI
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilimsaka Meninah na kumhoji juu ya sakata hilo la kutaka kuolewa na Diamond ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
“Yaani sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala hazina ukweli wowote.
“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye. Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye jambo ambalo si la kweli.”
“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.”
Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.TUJIKUMBUSHE
Kwa wiki kadhaa sasa, Meninah na Diamond wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni