Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu, Amama mbabazi na kumteua Dk Ruhakana Rugunda kushika wadhifa huo .
Taarifa elekezi ya Rais Museven kwenda kwa spika wa Bunge Rebecca
Kadaga, kwa njia ya barua imeeleza nia ya mabadiliko hayo na
kuambatanisha pia uteuzi wa Dk Rugunda
Rais Museven amemshukuru Mbabazi kwa mchango wake kwa nchi ya Uganda
tangu mwaka 2011 akieleza kuwa ujuzi na uongozi bora aliokuwa nao
utaendelea kuigwa na kuwa chachu ya uongozi bora kwa manufaa ya watu wa
Uganda
Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais
Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo
uhusiana kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.
Mapema mwaka huu
chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni
ambaye amekuwa kiongozi kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wake wa
pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mmewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
chanzo; mwananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni