Jumla ya Mara Iliyotazamwa

26 Sep 2014

MENINAH AFUNGUKA TENA JUU YA TETESI ZA KUFUNGA NDOA NA MSANII DIAMOND PLATINUMZ


YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada
Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kikizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond.
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
Ilisemekana kwamba baada ya Wema kuzinyaka habari hizo kuwa anataka kunyakuliwa ‘beibi’ wake mbaya zaidi wanataka kufunga ndoa, malkia huyo mkubwa wa sinema Bongo aligeuka mbogo na kuanza kuweka mikakati ya kumteketeza Meninah asiweze kufunga ndoa na Diamond.
Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem.
Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star 
Kuna madai kwamba Meninah aliposikia Wema anamsaka usiku na mchana ili amshikishe adabu, msanii huyo alishtuka kwa kuwa anaujua vizuri ‘mziki’ wa staa huyo.
Diamond
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
VIKAO VYA HARUSI VYAFANYWA
Taarifa ziliendelea kudai kwamba, vikao vya harusi vya chinichini vinaendelea kufanywa huku wahudhuriaji wakiwa ni mdogo wa Diamond ambaye pia ni mwanamuziki, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darlin’ pamoja na baadhi ya ndugu wa upande wa mama Diamond ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa.
POMBE NA STAREHE VYATAJWA
Sababu kubwa inayosemekana Wema kutemwa kuolewa na Diamond ni kutokana na kuendekeza pombe na starehe jambo ambalo Meninah yupo nalo kando na kwamba hivi sasa amekuwa akitimba kwa mama Diamond bila wasiwasi huku akizama jikoni kupika, kupakua na kufanya kazi ndogondogo za ndani ili kuthibitisha kuwa yeye ni mama bora.
DIAMOND AMTOA MACHOZI
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilimsaka Meninah na kumhoji juu ya sakata hilo la kutaka kuolewa na Diamond ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
“Yaani sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala hazina ukweli wowote.
“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye. Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye jambo ambalo si la kweli.”
“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.”
Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.TUJIKUMBUSHE
Kwa wiki kadhaa sasa, Meninah na Diamond wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

20 Sep 2014

Rais Museveni amfuta kazi Waziri mkuu



Waziri Mkuu aliyeteuliwa DK Ruhakana Rugunda (kushoto) ambaye amebadili nafasi Amama mbabazi (Kulia).


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu, Amama mbabazi na kumteua Dk Ruhakana Rugunda kushika wadhifa huo .

Taarifa elekezi ya Rais Museven kwenda kwa spika wa  Bunge Rebecca Kadaga, kwa njia ya barua imeeleza nia ya mabadiliko hayo na kuambatanisha pia uteuzi wa Dk Rugunda

Rais Museven amemshukuru Mbabazi kwa  mchango wake kwa nchi ya Uganda tangu mwaka 2011 akieleza kuwa ujuzi na uongozi bora aliokuwa nao utaendelea kuigwa na kuwa chachu ya uongozi bora kwa manufaa ya watu wa Uganda

Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo uhusiana kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.

Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa kiongozi kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wake wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.

Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mmewe ameonewa.

Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.

chanzo; mwananchi

ALIKIBA AFUNGUKA KUHUSU IDADI YA WATOTO ALIONAO NA MAISHA YAO



Mmoja kati ya watoto wa Alikiba!Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema kuwa ana watoto watatu na kila mmoja ana mama yake.


Msanii anayetamba na nyimbo ya Mwana, Alikiba!
Akizungumza na jarida moja la burudani kiba aliyetoa nyimbo mbili mpya hivi karibuni alisema kuwa kati ya watoto hao mmoja anaishi nae, wa pili yupo Dar es salaam na mama yake na wa tatu anaishi Uingereza na mama yake.

SERENGETI FIESTA IRINGA JANA USIKU NI SHANGWE ZA KUTOSHA



Wakazi wa Iringa usiku wa September 19 walipata burudani ya shangwe za Serengeti Fiesta 2014 iliyofanyika katika viwanja vya Samora mjini humo. Jionee picha za show hiyoMadee aka Rais wa Manzeshe akitumbuiza



Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wakiimbia kwa hisia hit yao ‘Me and You’



Mshindi wa super diva mkoani Iringa ambaye ni mlemavu wa macho


Makomando wakipiga salute



Linah akijiachia jukwaani


Juma Nature aka Kibra


Backstage: Linah, Juma Nature, Vanessa Mdee na Adam Mchomvu





Backstage: Linah na Edo Boy


Ommy Dimpoz, B12, Linah na wasanii wengine wakiwa jukwaani


Juma Nature na wasanii wenzake wa TMK Halisi wakifanya mambo


Mzee wa Hisia: Afande Sele akitumbuiza


Afande akiimba kwa hisia kali


Baba Levo


Peter Msechu




Godzilla aka Zizi


Adam Mchomvu na Godzilla


Me and You: Vanessa na Ommy Dimpoz


Ommy Dimpoz


Dogo Janja


Madee na vijana wa Tiptop Connection


Madee



Linah na dancers wake


Young Killer na hype man wake


Kabayser


Vanessa Mdee akiwa na dancers wake










Wasanii wote walipanda jukwaani kuonesha upendo wakati Juma Nature alipokuwa akifunga show


B12




Nickson George



Mo Music


Barakah Da Prince