Jumla ya Mara Iliyotazamwa

16 Ago 2014

SOMA HAPA UCHEKI DHARAU YA MENINA KWA DIAMOND NA WEMA


Screen Shot 2014-08-15 at 2.22.56 PM
Mwanzoni mwa wiki hii kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kulisambazaa taarifa za Meninah kuhusishwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake ambae ni Diamond Platnumz ambapo kupitia Leo Tena ya Clouds Fm Meninah amekubali kuongelea hii.
 Matano aliyoyasema Menina ni haya hapa chini…
 1.Sina uhusiano wowote na Diamond Platnumz.
 2.Mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa Dodoma kwenye uzinduzi wa video ya Miaka 50 ya Muungano.
 3.Sijawahi kuwasiliana nae hata namba yake ya simu sina kwenye simu yangu.
 4.Mimi napenda uhusiano wao kati yake na Wema Sepetu.
 5.Nampenda Wema kama dada yangu na namkubali Diamond Platnumz kama msanii mwenzangu.


HA HA HA UWOYA AFUNGUKA KWA NINI HAPENDI KUVAA CHUPI


mrembo na staa wa filamu nchini Irene
Uwoya amesema kuwa hakuna vazi
asilolipenda kulivaa kama chupi a.k.a
kufuli. Irene amesema hayo alipokuwa
akizungumza na magazine maarufu ya
burudani ya VIBE.
Alipoulizwa na mwandishi wa jarida hilo kuwa ni
nguo gani ni vigumu kuikuta kwenye kabati lake,
“ Chupi – sipendi kabisa hilo vazi” Alisema Irene
uwoya.

15 Ago 2014

MAKAMANDA WA MATAWI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM KATA YA KIMANGA WALIVYOSIMIKWA

Dotto Mwaibale
VIJANA nchini wametakiwa kuwa makini kwa kutumiwa na wanasiasa ili kuvuruga amani na usalama wa nchi uliodumu kwa muda mrefu.

Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Khamis Juma Sadifa wakati wa hafla ya kuwasimika makamanda tisa wa umoja huo wa matawi katika Kata ya Kimanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Ninyi vijana ndio walengwa wakubwa kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani na usalama wa nchi hivyo kuweni makini katika jambo hilo kwani tunachokihitaji ni amani na usalama wa nchi kwa watu wote na itikadi za vyama vyetu" alisema Sadifa

Sadifa alisema hata nchi hii ikitokea kuongozwa na chama kingine lakini bila ya kuwa na amani ni kazi bure hivyo ni vema kila mmoja wetu akatambua kuwa hana budi kuilinda amani iliyopo na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine Sadifa alitoa baraka zake kwa Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, Scollastica Kevela kuendelea na utendaji kazi wake wa kuinua uhai wa chama katika kata yake kwa kuwatembea vijana na wanachama ili kujua changamoto zinazo wakabili.

"Nakuomba kamanda wangu Kevela endelea kufanya kazi yako ni kuimarisha chama katika matawi kwa kukukutana na vijana na si kukiuka sheria ya kuanza kufanya kampeni kama inavyodaiwa" Sadifa alitoa onyo.

Sadifa aliongeza kuwa kazi kubwa ya ukamanda wa vijana ni kuwakutanisha vijana na kusikia changamoto walizonazo na kuziwakilisha ngaji ya juu kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake Kevela alisema kazi ya kuwainua vijana kiuchumi ndio kipaumbele chake cha kwanza na atahakikisha anafanya hivyo kupitia vikoba ambako yeye ni Makamu wa Rais wa chama hicho nchini.

Alisema amekuwa akifanya ziara katika matawi mbalimbali kwenye kata yake ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kuimarisha chama hangamoto zinazowakabili vijana hao.


Katika hafla hiyo Sadifa alitoa vifaa vya michezo jezi na mipira kwa vilabu mbalimbali vya matawi katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wa ofisi ya CCM katika eneo hilo ambapo zaidi ya sh. 500,000 zilipatikana.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, akielekea meza kuu tayari kwa shughuli ya kusimika makamanda hao.
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kusimikwa kwa makamanda tisa wa vijana wa matawi katika Kata ya Kimanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Ilala, Alfred Tukiko.Makamanda tisa wa Matawi Kata ya Kimanga wakila kiapo baada ya kusimikwa.

HALI YA AFANDE SELE SI NZURI BAADA YA KUFIWA NA MAMA WA WATOTO WAKE


Msanii wa Bongo Fleva,Afande Sele hali yake imekuwa mbaya baada ya kufiwa na mzazi mwenziye Asha Mohamed’Mama Tunda’.Msanii huyo inawezekana akawa ni moja kati ya watu maarufu hapa nchini ambao wanaongoza kwa kuwataja wenza wao sehemu tofauti tofauti ambapo zaidi ya miaka 10 amesikika akimtaja wa ubavu wake, mara kwa mara hiyo ni wakati wakiwa wanaishi pamoja na mama tunda ambaye ni mzazi mwenzake waliyezaa nae watoto wawili, wa kwanza ni Tunda pamoja na Asante Sanaa. Mama Tunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, na kabla ya kifo chake alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya malaria pamoja na pumu, mazishi ni leo saa tisa mchana,hata hivyo clouds fm imezungumza na msanii wa karibu wa Afande Sele,MC Koba baada ya Afande Sele kushindwa kuzungumza kutokana na hali yake kuwa mbaya.




RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA DIASPORA JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua tovuti rasmi ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014.
Pamoja naye ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Taasisi ya Diaspora Bw. Emmanuel Mwachullah (wa pili kulia), Mwana-Diaspora Dennis Londa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Rose Jairo


PICHA NA IKULU

22 Jun 2014

WAFUMANIA NYAVU BORA
 Kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo utamu wa kombe la dunia unapozidi kuongezeka na hiyo ni kutokana na kiatu cha dhahabu kugombaniwa na wachezaji mbalimbali bila kujali ukubwa wa timu.
Katika fainali za kombe la dunia la mwaka 2010 kule Afrika Kusini, Thomas Muller ndiyo alikuwa mfungaji bora na bado kwa mwaka huu mpaka sasa yupo katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa na magoli matatu aliyopiga hat trick katika mechi yao dhidi ya Ureno wakipowavurumishia mvua ya mabao manne.
Wachezaji wengine wenye mabao matatu ni Robin Van Persie na Arjen Robben wote wa Uholanzi, Karim Benzema wa Ufaransa pamoja Enner Valencia wa Ecuador.
                                                  WASHAMBULIAJI WANAOONGOZA.
Enner Valencia ndiyo mshambuliaji aliyeshitua watu kutokana na kutofahamika kwake sana ukilinganisha na wafungaji wengine kwani anachezea klabu ya Pachuca katika Liga MX. 
Lakini kama kawaida maswali kwetu hayaishi na tunajiuliza je Thomas Muller atatetea ufungaji bora wa dunia au naye atashindwa kutetea kama Uhispania ilivyoshindwa kutetea kombe na kutolewa kwa aibu.
                                 Imeandikwa na Neligwa Mugittu (Nellynice Mnyiramba).

RONALDO, KLOSE MAPACHA WASIOFANANA.

RONALDO DE LIMA, KLOSE MAGWIJI WA NYAVU.
 Licha ya tofauti za mechi walizocheza na utofauti wa Utaifa wao Ronaldo De Lima pamoja na Miroslav Klose ndio wababe wa kuwatesa makipa katika kombe la dunia.
Ronaldo alishastaafu kucheza soka akiwa ameweka rekodi ya kufunga goli 15 katika fainali mbalimbali za kombe la dunia ambaye alitania kwa kuwaambia Wabrazil wamuombee Klose aumie ili asiweze kumfikia na kumpita rekodi yake aliyoiweka.
Katika fainali za mwaka huu zinazofanyika katika nchi ya Ronaldo ndipo Klose kaifikia rekodi ya Ronaldo na bado mechi zipo za kumfanya ampite kabisa.

                          REKODI KATI YA KLOSE NA RONALDO KATIKA KOMBE LA DUNIA.
Pamoja na kufanana kwa rekodi hiyo pia timu ya Afrika GHANA imeingia katika rekodi wa wabaya wa makipa hao kwa kuwa timu iliyofungwa katika goli zao za 15.
                                             KLOSE NA RONALDO DHIDI YA GHANA.
Cha ajabu katika fainali zote nne za Miroslav Klose hajabadilisha aina yake ya ushangiliaji pindi anapoinyanyasa timu pinzani kwani upendelea kuruka sarakasi.
                                                      USHANGILIAJI WA KLOSE
Swali lililobakia katika vichwa vya watu ni je Miroslav Klose atakuwa mfungaji bora wa kipindi chote katika kombe la dunia na kufanikiwa kumpita Ronaldo De Lima?
Swali ilo ni gumu kulijua kwani hakuna aijuae kesho hivyo ni suala la muda na uzima kusubiri kuona rekodi hiyo kama itavunjwa.
                                     Written by Neligwa Mugitttu (Nellynice Mnyiramba)