Jumla ya Mara Iliyotazamwa

29 Ago 2014

BODABODA IRINGA WAWALIZA CHADEMA WAZIDI KUDHIHIRISHA KWAMBA WAO NI CCM DAMU

madereva bodaboda wa mjini Iringa wakiingia uwanjani
wakionesha shamrashamra katika sherehe hizo

Mwigulu Nchemba akimuongoza Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Salim Asas kuwapongeza bodaboda hao
Nchemba akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodaboda Mjini Iringa, Mwmbope Joseph
MWENYE macho aaambiwi tazama; hivi ndivyo unavyoweza kuzizungumzia sherehe za kumuapisha Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Salim Abri maafuru kwa jina la Salim Asas.

Wale vijana machachari wa barabarani, ambao hivi karibuni walijinasibu mbele ya kadamnasi kwamba wao ni CCM damu jana katika sherehe hizo wamedhihirisha tena kauli waliyoitoa kwenye kikao chao na uongozi wa SUMATRA kilichofanyika hivikaribuni kwamba wao ni CCM.

Vijana hao si wengine zaidi ya wale wanaojulikana saaaana kwa kupamba misafara ya viongozi wa kisiasa. Ni vijana wanaogombaniwa na vyama vyote vya kisiasa, ni vijana wanaelezwa kuwa mtaji mzuri wa kisiasa pamoja na kwamba hawatabiriki, hao si wengine ni madereva wa vyombo vya usafirishaji vya miguu miwili na mitatu (bodaboda na bajaj).

Jana walikuwepo kwa mamia. Walizunguka mji mzima wa Iringa wakiwa na bodaboda na bajaj zao, wakiwa wamevaa sare ya kijani ambayo ni vazi rasmi la CCM.

Msafara wao mrefu ulivutia wananchi wa mjini hapa, wakajitokeza kwa wingi barabarani kuona msururu wao na jinsi walivyokuwa wakiendesha vyombo vyao kwa mbwembwe.

Wakasaidia kuwavuta watu waliokuwa hawajui au waliojifanya wameziba masikio kwamba hawajasikia Asas, kipenzi cha wakazi wa Iringa, anaapishwa kwa awamu ya tatu kuwa kamanda wa UVCCM.

Wakiwa na Kamanda Mteule, Asas na mgeni rasmi wa sherehe hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba walishiriki uzinduzi wa matawi mapya ya CCM zaidi ya matano mjini hapa.

Na baadaye wakaongoza msafara wa viongozi hao kuelekea uwanja wa Mwembetogwa ambako sherehe za kumuapisha Asas zilikuwa zikifanyika.

Pamoja na Bodaboda palikuwa na burudani nyingine tosha, iliyopamba sherehe hiyo ambayo Asas mwenyewe aliita ni sherehe ya aina yake ambayo haijawahi kutokea katika historia yake ya kisiasa.

Ilikuwepo bendi ya muziki wa dansi ya Vijana Jazz na wasanii wengine akiwemo Dokii na kundi lake, Makomandoo, Baba Level, Wanne Star na wasanii kibao wa mjini Iringa.

Mbali na wasanii hao kuwa gumzo kwa burudani waliyotoa katika sherehe hizo, bodaboda walinogesha zaidi gumzo hilo.

“Wametukimbia, wametukimbia kwasababu ya ubishi wa ndugu yetu Msigwa, Mchungaji Peter Msigwa anataka kutupa kazi ngumu ya kusaka kura 2015,” alisema mmoja wa vijana wa kijiwe cha stendi kuu.

Kijana huyu hajasikika, akapaza sauti yake, ili Mchungaji Msigwa aisikie akisema……TUMEKWISHA.

Bodaboda wana matatizo makubwa pamoja na kwamba ni mtaji mkubwa wa kisiasa. CCM inawasaidia, iko jirani nao kwa raha na shida lakini sisi tunasubiri tuwaite kwenye mikutano, tena kwa kuwapa elfu tano tano. Wapi na wapi? ASIYESIKIKA huyo alisema.

ASIYESIKIKA mwingine akasema walileta matatizo yao kwetu Chadema na CCM. Wenzetu CCM wakawa wajanja, wamewatekelezea japo siyo yote lakini inawapa matumaini kwamba wamesikilizwa.

Ndio wenzetu CCM nasikia waliwapa mafunzo ya udereva ili wajue sheria za barabarani. Zaidi ya madereva 800 wamefundishwa bila kuchangia hata senti tano, wakatafutiwa ofisi, wakaanzisha chama chao, wakapema mtaji wa zaidi ya Sh Milioni tano kwa ajili ya kuanzisha Saccos yao na wakapewa pikipiki nne kwa ajili ya kukopeshana kwa mzunguko.

Sisi tumebaki na maneno, kila kukicha ni kulalama tuuu Peoples Power…. People Power… halafu tuko mbali na maendeleo ya watu, nani atatuthamini? Tuoneshe basi kwamba tunajali matatizo ya watu, tujitokeze kuwasaidia sio tu kwa kusubiri fedha za serikali na kwa kutumia fedha zetu maana hakuna serikali inayoweza kutatua matatizo ya watu wake wote, hiyo ni ndoto hata kwa mataifa tajiri.

ASIYESIKIKA mwingine akasema wanachofanyiwa na CCM kinaongeza gharama; hatutawapata kirahisi tena katika misafara ya viongozi wetu……watata ujira uongezeke, nani atatoa…… hilo linabaki swalia kwa wengi wetu
na fredy mgunda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni