MBONGO-Fleva
anayefanya poa na ngoma yake ya Nitasubiri, Juma Mussa ‘Jux’ na staa
mwenzake ambaye ana kofia nyingine ya utangazaji, Vanessa Mdee ‘V-Money’
wanadaiwa kuwa ni wapenzi.
Juma Mussa ‘Jux’ akiwa na Vanessa Mdee ‘V-Money’ wanaodaiwa kuwa ni awapenzi.
Madai ya wawili hao kuhusishwa
kimapenzi yameendelea kujidhihirisha siku hadi siku na zaidi ni hivi
karibuni walipokutana kwenye ziara ya Serengeti Fiesta 2014 mkoani
Kagera na Tanga, ambapo muda mwingi walionekana kugandana kama luba hadi
wenzao kudai kuwa walikuwa hata wakilala chumba kimoja hotelini.
Katika kuwafuatilia, paparazi wetu
alifanikiwa kupata baadhi ya picha za matukio yao yaliyoonesha michakato
na harakati zao za kimalovee zinavyokuwa siku zote.
Wakiteta jambo.
Jux na Vanessa, wakiwa mkoani humo
walionekana muda mwingi wakiwa pamoja kwenye gari walipokuwa wakienda
kumuona Babu Njenje na wakati wakiwa wanaelekea Uwanja wa Mkwakwani
kwenye shoo.
Hata baada ya Jux kushuka stejini,
alionekana akiwa amekaa ‘very close’ na Vanessa huku wakiwa kwenye
mazungumzo yaliyodaiwa ni ya kimahaba niue.
Wakiwa pamoja kama kumbikumbi.
Mpaparazi alifanya jitihada za
kuzungumza na Jux juu ya uhusiano wao, lakini jamaa huyo alimchomolea
kwa kusema kwamba hayuko tayari kuzungumzia ishu hiyo kwani Vanessa ni
mshikaji wake tu na hakuna kibaya juu yao zaidi wanafanya kazi pamoja
tu.
“Kiukweli sihitaji kuzungumza lolote
juu yangu na Vanessa ila ni mwanamuziki mwenzangu hivyo tunafanya kazi
pamoja,” alisema Jux.Vanessa kwa upande wake alipoulizwa juu ya ishu
hiyo, alimtaka mpaparazi ‘kuipotezea’ habari hiyo kwani si muhimu kwa
sasa.
Mbali na Vanessa, Jux aliwahi kudaiwa
kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper na modo Jacqueline Patrick huku
Vanessa naye akiwa alisharipotiwa kutoka na Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
jux na modo Jacqueline Patrick
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni