Jumla ya Mara Iliyotazamwa

25 Ago 2014

KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA VICHEKESHO LA "ORIJINO KOMEDI",MASANJA MKANDAMIZAJI AFUNGUKA



Baada ya miaka kadhaa ya kutamba kwa kundi la vichekesho la Ze Komedi kisha kudaiwa kusambaratika, mmoja wa memba wa kundi hilo, Emmanuel Mgaya ‘ Masanja Mkandamizaji’ ameibuka na kueleza kutokana na ishu nzima.

 Masanja ambaye pia ni mchungaji amefunguka na kueleza kila kitu kuhusiana na ishu hiyo huku akikanusha vikali kuwepo kwa uvunjifu wa kundi hilo. 

Akizungumza na mwandishi wetu, Masanja alisema kuwa kundi hilo halijavunjika kama ilivyoripotiwa na kudai kuwa litarejea kama kawaida kuanzia mwezi Septemba mwaka huu na kuendelea kubamba kama ilivyozoeleka kipindi cha nyuma na kufanikiwa kujizolea umaarufu wa kutosha nchini.

 “Kikubwa tu watu waachane na hizo tetesi Ze Komedi kwamba imevunjika, nasema kwamba haijavunjika wala hatujasambaratika hata kidogo, tupo na tutaendelea kuwepo. Rasmi tutaanza kazi Septemba mwaka huu,” alisema Masanja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni