Jumla ya Mara Iliyotazamwa

26 Ago 2014

Ukiona mpenzi wako ana tabia hizi, kimbia fasta !!!

Jambo la kumuacha au kutomuacha mpenzi wako linaweza kuwa bado gumu kwa asilimia kubwa ya wadada, hasa pale mtu anapokuwa amezama teyari katika mapenzi, haijalishi umepata ushahidi kiasi gani au umeshuhudia maovu mangapi ukifanyiwa, bado suala hili ni gumu kupata jibu sahihi mara nyingi. Wapenzi wengi wanaona ni vigumu kufikia maamuzi kutokana na mazoea tu, ila kuna dalili ambazo ukiona mpenzi wako akifanya, anza kukimbia mapema tu kabla ujazidi kuzama, na kupoteza mlango wa kutokea.
Hatimizi kila anachoahidi.
Mapenzi huanza na uaminifu, tena uaminifu unaanzia kwenye vitu vidogo sana, moja yapo ni pale anapokuahidi atakupigia simu muda flani, unaweza kusubiri hadi jua linazama, bila hata ya kukutarifu kilichomsibu, inatokea mara nyingi labda kazi nyingi zinafanya mtu asahau, ila kama ndio tabia sasa kusahau.basi hauna umuhimu katika maisha yake.
hatimizi-ahadi
Anamuongelea mpenzi wake wa zamani mara kwa mara.
Kwa mwanaume anayemuongelea mpenzi wake wa zamani, hapo kuna mawili, bado anampenda sana au anamchukia, vyovyote vile itakapoangukia, hii inamaanisha hajamalizana na mpenzi wake wa zamani kwa hiyo, ni vigumu kukupa 100% zote kwako.
wanabishana-wapenzi
Anakusaliti mara kwa mara
Mapenzi yanapokuwa bado machanga, unakuta watu hawaachani, kila sehemu wapo wote, mbaya zaidi unapogundua kuwa mpenzi wako anakusaliti mapema yote hii, jiulize haswa ni nini kitakachokuwa kinaendelea hapo baadae.
mpenzi-ana-cheat
Anakupelekesha, hasa inapotokea wakati bado mapenzi machanga.
Watu wengine wanatabia ya kuendesha wenzao jinsi anavyotaka yeye, hasa kwa wapenzi wengi, mfano mdogo unakuta wakati ndio kwanza mmeanza kutoka, atataka uanze kubadili jinsi uishivyo,mfano atataka uanze kubadilisha jinsi unavyovaa, anategemea uwepo kwa ajili yake masaa yote, anataka kujua kila mwenendo wako, anataka upungue uzito, uachane na marafiki zako na mengine mengi.
mpenzi-ananipelekesha
Kama rafiki zako wote wa karibu wakikuonya kuwa huyo ni kicheche.
Siku zote lisemwalo lipo, hata kama upo umezama kiasi gani katika mapenzi, rafiki zako wa karibu siku zote ndio watakaoanza kukupa ukweli hata kama hutaki kusikia, kama kila rafiki wako wa karibu anadhani kuwa jamaa siyo mtu mzuri, au ni kicheche, kuna asilimia 98% kuwa ni kicheche kweli.
mpenzi-anaonywa

Maoni 1 :