Jumla ya Mara Iliyotazamwa

27 Ago 2014

MSANII AKOMBA VITU KWA BWANA’KE


Fatma Leonard 'akila kona'.
MSANII wa filamu Bongo, Fatma Leonard wiki iliyopita alinaswa na paparazi wetu akihamisha vitu vya ndani nyumbani kwa mpenzi wake huko Ubungo Makuburi jijini Dar es Salaam akidai kuchoshwa na maisha bila ndoa. Hata hivyo, paparazi lilikuta tayari mzigo wa fenicha umeshaondoka.
Msanii wa filamu Bongo, Fatma Leonard akifungasha virago kuianza safari.
“Nimemvumilia kwa muda mrefu sana, kila siku namkumbusha, sasa inaonekana kama ninalazimisha, nimeamua kuchukua vyangu kwa sababu nimempata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye yupo tayari kunioa,” alisema Fatma akikataa kulitaja jina la mpenzi wake huyo anayempotezea muda.
Baba mwenye nyumba hiyo alimpigia simu mpangaji wake kumfahamisha kuhusu kuondolewa kwa mizigo hiyo, lakini alimtaka amuache achukue anachotaka, kitu kinachoonyesha aliridhia kitendo hicho kilichowavutia majirani wengi waliojazana kushuhudia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni