Beyonce, Jay Z na binti yao Blue Ivy au waite The Carters, Jumapili (Agosti 24) kwenye tuzo za MTV VMA wameendelea kuthibitisha kuwa ni ‘happy family’ licha ya ripoti mbalimbali ambazo zimeendelea kutolewa kuhusu matatizo ya ndoa yao.
Beyonce alishinda tuzo ya ‘Michael Jackson Video Vanguard Award’ kwenye tuzo za MTV VMA 2014.
Lakini kubwa zaidi ni pale ambapo familia yake Jay Z na binti yao Blue Ivy waliopanda jukwaani na kumkabidhi (mke/mama) tuzo hiyo, kisha baba na mama wakapeana busu jukwaani. Queen Bey aliipokea tuzo hiyo akitoa machozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni