Jumla ya Mara Iliyotazamwa

27 Ago 2014

KHADIJA KOPA AWACHANA WASIOHESHIMU WAUME KWA USUPASTAA WAO


MALKIA wa muziki wa Taarab Afrika Mashariki, Khadija Omary Kopa amewachana mastaa wa kike wasioheshimu waume zao kwa usupastaa wao, akisema suala hilo limewafanya washindwe kudumu katika ndoa zao.
Malkia wa muziki wa Taarab Afrika Mashariki, Khadija Omary Kopa.
Malkia huyo alitoa dongo hilo juzikati wakati alipokuwa akipagawisha mashabiki wake katika ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori jijini Dar alipokuwa jukwaa moja na bendi ya Extra Bongo, akiimba nyimbo zake mbili za Fahari ya Mwanamke na Full Stop.
“Mwanamke unajiona staa mbele ya mumeo kisa supastaa, eti inafikia hatua  hadi unaachika! mwanamke unapaswa uwe na heshima kwa mumeoeeee!”alisema mkali huyo na kuitikiwa kwa shangwe na mashabiki wake kibao waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni